Pata taarifa kuu
UGANDA

Besigye afikishwa Mahakamani kwa kupuuza polisi

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Uganda FDC, Kizza Besigye amefikishwa katika Mahakama ya Kasangati jijini Kampala, alikoshtakiwa kukeuka maagiza ya polisi.

Kizza Besigye kiongozi wa upinzani nchini Uganda
Kizza Besigye kiongozi wa upinzani nchini Uganda Chimp reports
Matangazo ya kibiashara

Usalama umeimarishwa ndani na nje ya Mahakama hiyo, huku wakionekana kila kona wakiwa wamejihami.

Wafuasi wa FDC wamefurika katika Mahakama hiyo kusikiliza kesi dhidi ya kiongozi wao.

Kiongozi wa mashtaka katika kesi hiyo amewasilisha mkanda wa video ukionesha namna Besigye alivyokaidi agizo la polisi kwa kutopitia barabara maalum aliyokuwa ametengewa na polisi na badala yake akaamua kupitia katikati ya jiji la Kampala wakati alipokuwa anaenda kwenye makao makuu ya chama chake katika eneo la Najjanankumbi.

Mbali na kesi hii, Dkt  Besigye pia ameshtakiwa kwa kosa uhaini katika Mahakama ya Nakawa baada ya kujiapisha kama rais wa nchi hiyo baada ya uchaguzi Mkuu wa mwezi Februari aliodai kushinda.

Besigye, anasema kesi dhidi yake ni za kisiasa wakati huu akiendelea kuzuiliwa katika Gereza la Luzira.

Wabunge wa upinzani wamekuwa wakimtaka rais Yoweri Museveni kuagiza kuachiliwa huru kwa Besigye ambaye alikuwa daktari wake wakati wa vita vya msituni miaka ya 80, lakini kiongozi huyo amesema hana mamlaka ya kuingia uhuru wa Mahakama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.