Pata taarifa kuu
TANZANIA-URAIS

Rais Magufuli atimiza siku mia moja uongozini

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, anatimiza siku mia moja toka aingie madarakani, huku asilimia kubwa ya wananchi wakioneshwa kuridhishwa na utendaji wake. Wadau mbalimbali wamempongeza rais Magufuli kwa mbinu na kasi ya uongozi katika serikali ya awamu hii ya 5, huku kukiwa na wengine ambao wakimkosoa hususan kuhusu utekelezaji wa ahadi zake.

John Pombe Joseph Magufuli wakati akiapishwa kuwa rais Novemba 5, 2015.
John Pombe Joseph Magufuli wakati akiapishwa kuwa rais Novemba 5, 2015. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mambo aliyoanza kuyashughulia punde baada ya kuingia madarakani ni pamoja na ukusanyaji wa kodi, kudhibiti vitendo vya rushwa, kuboresha huduma za afya, elimu na kubana matumizi ya fedha za Serikali, fedha ambazo nyingi amezilekeza kwenye shughuli za maendeleo.

Lakini licha ya mafanikio haya ndani ya siku mia moja, wachambuzi wa mambo wanaona kuwa bado kuna chagnamoto zaidi ambazo zinamkabili na mabazo huenda akachukua muda kuzikabili.

Suala la ushirikiano wa kimataifa na safari za nje ni eneo jingine ambalo baadhi ya watu wamepongeza kwa kupunguza safari za viongozi wa Serikali ambapo sasa watahitaji kibali chake ili kuwaruhusu kusafiri nje.

Wapo pia wanaohoji ni kwanini rais Magufuli hajahudhuria mikutano ya wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika iliyofanyika hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.