Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Idara ya Usalama Somalia yaonyesha sehemu ya uchunguzi wa mlipuko wa bomu

Idara ya usalama nchini Somalia imeonyesha hapo jana picha za video zinazo muonyesha mtu mmoja anaeshukiwa kutega bomu lililolipuka ndani ya ndege ya kampuni ya Daallo Airlines iliolazimika kutuwa kwa dharura jijini Mogadishu.

Ndege ya kampuni ya Daallo Airlines
Ndege ya kampuni ya Daallo Airlines
Matangazo ya kibiashara

Mtu huyo anaonekana akibeba begani kompyuta ndogo ya mkononi inayoaminika kuwa ndio iliowekwa bomu ndani yake baada ya kukabidhiwa na watu wengine wawili ambapo mmoja alikuwa akivalia jaketi ya usalama na ambaye anaonekana pia kwenye mkanda huo wa video, kulingana na kituo cha Usalama nchini Somalia.

Takriban watu 15 wametiwa mbaroni wakishukiwa kuhusika katika tukio hilo la ajali ya dege. Kiongozi mmoja wa Somalia ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa bomu hilo lilikuwa limefichwa ndani ya kmputa ndogo ya mkononi iliokuwa miongoni mwa habiria wa ndege hiyo.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa, Kulingana na picha hizo za video zinaonyesha kuwa shambulio hilo liliratibiwa na kundi la watu ambao miongoni mwao wametiwa mguvuni na wengine wanafuatiliwa na vyombo vya sheria.

Baada ya kuelezwa kwamba mlipuko uliotokea katika ndege hiyo dakika 15 baada ya kuruka kutoka katika uwanja was Mogadiscio ulisababishwa na tatizo la hewa, lakini siku ya Jumamosi serikali ya Tanzania imekiri kuwa mlipuko huo ulisabishwa na bomu.

Mlipuko huo ulisababisha tundu na mita moja lenye mduara katika ndege A321 ya kampuni ya Daallo, inayo fanya shughuli zake kati ya Djibouti na eneo la pembe ya Afrika pamoja na nchi za Ghuba.

Habiria mmoja aliejulikana kwa jina la Abdulahi Abdisalam, ambae alitoweka hewani, aliordheshwa na viongozi wa Somalia kwamba aliuawa katika mlipuko huo, huku watu wengine wawili wakijeruhiwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.