Pata taarifa kuu
Kenya

Watu zaidi ya 50 wauawa katika mapigano ya wakulima na wafugaji Kenya

Zaidi ya watu 50 wameuawa katika Wilaya ya Tana River Pwani ya Kenya kutokana na makabiliano ya jamii mbili wafugaji na wakulima zinazotofautiana.Mauaji hayo yanaelezwa kuwa ya kulipiza kisasi kati ya jamii ya Orma na Pokomo, jamii zinazonga'nga'ngania malisho na maeneo ya kuchunga mifungo.

RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Inatuhumiwa kuwa wachunga wa jamii ya Ormna waliwavamia wakulima wa Pokomo na kuwajeruhi jambo ambalo wenyeji wa eneo hilo wanasema lilisababisha makablinao hayo ambayo wengi waliouawa walikuwa ni watoto na wanawake.

Naibu mkuu wa jeshi la polisi mkoani Pwani Robert Kitur amethibitisha mauji hayo amabyo ameeleza watu waliouawa walikawta kwa mapanga,kuchomwa moto na makaazi yao kubolewa.

Serikali ya Kenya kwa sasa imetuma helikopta ya kijeshi kwa usaidizi wa shirika la msalaba mwekundu kuwasafisriha watu wengine ambao waliojeruhiwa katika mapamabano na kuwasafisriha kwa vituo mbalimbali vya afya kupata matibabu zaidi.

Mbuge wa eneo hilo Danson Mungatana ameishtumu serikali kwa kutochukua hatu ya haraka kuzuia mapigano hayo,na kuitaka wizara ya usalama kutoa ttamko la serikali kuhusu janga hilo ambalo ni baya zaidi kuwahi kushudiwa katika wilaya hiyo.

Muungano wa viongozi wa Kiislamu nchini Kenya ukiongozwa na Sheikh Mohammed Khalifa umeshtumu makabiano hayo na kutaka serikali kuweka mipango ya kuzuia makabiliano kama hayo katik siku zijazo.

Polisi nchini Kenya inaanda mkutano wa amani kati ya jamii ya Pokomo na Orma siku ya Alhasmisi kuzileta pamoja.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.