Pata taarifa kuu

Rwanda: Paul Kagame anapuuzilia mbali utata kuhusu matamshi ya Macron nkuhusu mauaji ya Watutsi

Siku moja baada ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa dhidi ya Watutsi mwaka 1994 nchini Rwanda, Rais Paul Kagame amefanya mkutano na waandishi wa habari Jumatatu Aprili 8 asubuhi katika mji mkuu Kigali. 

Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Palais des Congrès de Kigali, Kigali, Rwanda, Jumatatu, Aprili 8, 2024.
Rais wa Rwanda Paul Kagame katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Palais des Congrès de Kigali, Kigali, Rwanda, Jumatatu, Aprili 8, 2024. © Brian Inganga / AP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Rwanda alijibu kwa maneno ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye, katika video, alisisitiza juu ya hitaji la "kuangalia siku za nyuma usoni", bila kurejelea nukuu iliyotumwa na rais kwa vyombo vya habari, ikionyesha kwamba Ufaransa "ingeweza kukomesha mauaji ya kimbari”. Mabadiliko haya yanaonekana zaidi na zaidi kama shida katika mawasiliano ya Élysée.

Hata kama hakusafiri kwenda Kigali Jumapili Aprili 7 kwa matukio hayo, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alijiunga na ukumbusho wa miaka 30 ya mauaji ya kimbari ya Watutsi kupitia ujumbe wa video. Ujumbe huu uliendana na ule uliotolewa katika mji mkuu wa Rwanda Mei 27, 2021, alipotambua jukumu "nzito" la Ufaransa katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi. Alisisitiza juu ya hitaji la "kuangalia siku za numa usoni",

Wakati huo huo Rais Paul Kagame amesema kwamba alikuwa na wasiwasi wa kile anachokiona kama kushindwa kwa Marekani kuyatambua mauaji ya Mauaji ya 1994 kama mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi walio wachache nchini humo.

Kagame amewaambia waandishi wa habari kwamba suala hilo lilikuwa ni "mada ya mazungumzo" walipokutana na rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton aliyeongoza ujumbe wa Marekani nchini Rwanda kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji hayo.

Raia wengi wa Rwanda walimkosoa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kwa kushindwa kuweka wazi kwamba mauaji hayo ya kimbari yaliwalenga Watutsi, alipoandika kwenye ukurasa wa X kuhusiana na maadhimisho hayo.

Kagame amesema anaamini alifikia makubaliano na maafisa wa Marekani muongo mmoja uliopita wa kutoyakosoa mauaji hayo wanapofanya kumbukumbu hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.