Pata taarifa kuu

Rwanda: Vyama viwili vikongwe vyatangaza kumuunga mkono rais Kagame

Nairobi – Vyama viwili vikongwe nchini Rwanda, Liberal na Social Democratic, mwishoni mwa juma vimetangaza kuwa vitamuunga mkono mgombea wa chama tawala cha Rwanda Patriotic Front, Paul Kagame, katika uchaguzi wa mwezi Julai mwaka huu.

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Liberal na PSD kihistoria ni washirika wa chama tawala, na viongozi wao wamehudumu katika nyadhifa tofauti serikalini, ambapo rais wa Chama cha Kiliberali Donatille Mukabalisa pia ni Spika wa Bunge.

Kagame, ambaye aliingia madarakani mwaka 2000, anaruhusiwa kisheria kugombea muhula mwingine kufuatia mabadiliko ya katiba ya mwaka 2015 yaliyopelekea kuondolewa kwa kizuizi cha muhula wa rais.

Pamoja na ukosolewaji kutoka nje kuhusu nafasi ya demokrasia kwenye taifa hilo, tume ya uchaguzi imeahidi kufanya uchaguzi huru na haki licha ya kukosekana kwa wapinzani wakuu kama Victoire Ingabire

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.