Baadhi ya raia wakosoa sanamu iliyozinduliwa kwa heshima ya Nyerere
Nairobi – Baadhi ya raia wa Tanzania, kupitia mitandao ya kijamii wamekosoa sanamu mpya iliyozinduliwa kwa heshima ya rais wa zamani Julius Nyerere, wakidai haifanani naye.
Imechapishwa:
Sanamu hiyo ilizunduliwa siku ya Jumapili, nje ya makao makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia.Viongozi kadhaa walihudhuria uzinduzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU), Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 18 Februari, 2024. pic.twitter.com/7CJeT1mLEV
— ikulu_Tanzania (@ikulumawasliano) February 18, 2024
Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa taifa hilo tangu ilipojipatia uhuru wake mwaka wa 1961 hadi 1985.
Anakumbukwa kwa kupigania haki za raia wa Afrika na hata wakati mmoja kuwa mwenyeji wa baadhi ya viongozi waliokuwa wanapigania uhuru wa nchi zao, ikiwemo Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji.
Mwaka uliopita, sanamu iliyozinduliwa kwa heshima ya rais wa zamani wa Zambia, Kenneth Kaunda, iliondolewa baada ya kukashifiwa na raia kwenye taifa hilo kwamba haikuwa inafanana na Kaunda.