Pata taarifa kuu
UWEKEZAJI-UCHUMI

Rwanda yafikia makubaliano na kampuni ya Rio Tinto kwa ajili ya uchimbaji madini ya lithiamu

Rwanda imetia saini makubaliano na kampuni kubwa ya uchimbaji madini inayomilikiwa na Uingereza pamoja na Australia ya Rio Tinto kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya lithiamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, washirika hao wawili wametangaza Jumatatu.

Kuingia kwa Rio Tinto sokoni "kunaashiria dhamira ya Rwanda ya kufungua zaidi uwezo wa sekta ya madini nchini".
Kuingia kwa Rio Tinto sokoni "kunaashiria dhamira ya Rwanda ya kufungua zaidi uwezo wa sekta ya madini nchini". AFP/ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

 

Makubaliano hayo yanaakisi "juhudi za serikali za kuiimarisha na kuifanya sekta ya madini ya Rwanda kuwa ya kisasa", amesema Yamina Karitanyi, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rwanda Mines, Petroleum and Gas Board, inayomilikiwa na serikali, katika taarifa ya pamoja kwa pande zote mbili. Kuingia kwa Rio Tinto sokoni "kunaashiria dhamira ya Rwanda ya kufungua zaidi uwezo wa sekta ya madini nchini humo", pia amesisitiza.

Kampuni ya Rio Tinto "inafuraha kushirikiana na serikali ya Rwanda na kuongeza uzoefu wake wa kimataifa ili kuharakisha utafutaji wa migodi ya madii ya lithiamu katika Mkoa wa Magharibi wa Rwanda," amesema Lawrence Dechambenoit, mkuu wa mambo ya nje wa kimataifa wa kampuni ya Rio Tinto.

Lithium ni nyenzo muhimu katika utengenezaji wa betri zinazotumiwa katika magari ya umeme, simu mahiri smartphones za na vifaa vingine vya kielektroniki.

Mwezii wa Agosti mwaka jana, Bi Karitanyi alisema katika mkutano kuhusu uchimbaji madini nchini Rwanda kwamba sekta ya madini nchini humo "iko kwenye njia" kufikia lengo lake la mapato ya dola bilioni 1 mwaka 2023.

Alifurahishwa hasa kwamba sekta hiyo kupata "ongezeko la ajabu la uzalishaji wa bati, tantalum na tungsten, dhahabu, lithiamu na vito vya thamani, na kufanya ongezeko la asilimia 45.6 ya mapato ya 'uuzaji wa madini nje ya nchi ikilinganishwa na mwaka jana'.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.