Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rwanda: Mfalme wa Jordan akamilisha ziara iliyoashiria kusainiwa kwa mikataba mipya

Mfalme wa Jordan Abdallah II alimaliza Jumanne hii, Januari 9, ziara rasmi iliyoanza Jumapili katika mji mkuu Kigali. Nchi hizi mbili zilitia saini kwenye mikataba kadhaa ya kiuchumi, na hivyo kupanua uhusiano wa nchi hizo mbili uliyozinduliwa katika miaka ya hivi karibuni.

Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan akiongea wakati wa ziara yake kwenye Jumba la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali mjini Kigali, Januari 8, 2024.
Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan akiongea wakati wa ziara yake kwenye Jumba la Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali mjini Kigali, Januari 8, 2024. via REUTERS - ROYAL HASHEMITE COURT
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

Miongoni mwa wajumbe wa Mfalme Abdullah II mjini Kigali: Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jordan na Mkurugenzi wa Ujasusi. Ziara ya siku tatu ambapo mikataba kadhaa ya nchi mbili ilitiwa saini, ikiwa ni pamoja na mkataba wa kodi ili kuepuka utozaji kodi maradufu na mikataba ya maelewano ya ushirikiano katika sekta ya uchumi na kilimo.

Katika miaka michache, ziara rasmi zilifuatana kati ya viongozi wa nchi hizo mbili. Kwanza mnamo mwaka 2018 na 2022 na ziara za Rais Paul Kagame nchini Jordan kuhudhuria mikutano ya mchakato wa Aqaba, mpango ulioanzishwa na Mfalme Abdullah II wa kuimarisha uratibu wa kimataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Mnamo mwezi wa Februari 2023, ilikuwa zamu ya Naibu Waziri Mkuu na maafisa mbalimbali wa jeshi la Jordan kuwatembelea wenzao wa Rwanda mjini Kigali. Mkutano ulifuatiwa, miezi michache baadaye, na ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Vincent Biruta kwenda Amman mwez Agosti mwaka uliyopita, kwa ajili ya kutia saini mikataba mitatu, ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa visa kwa raia wa nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.