Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Rwanda: Uchaguzi wa urais kufanyika Julai 15, 2024

Raia wa Rwanda wameitwa kupiga kura Julai 15, 2024 kumchagua rais wao mpya, mkuu wa sasa wa nchi Paul Kagame akiwa mgombea kwa muhula wa nne, na kuchagua wabunge wao, Tume ya Uchaguzi imetangaza siku ya Jumanne.

Paul Kagame alikuwa na umri wa miaka 36 pekee wakati chama chake, Rwandan Patriotic Front (RPF), kilipowaondoa Wahutu wenye msimamo mkali kutoka madarakani, wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ambayo yaligharimu maisha ya watu 800,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hasa Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani, kati ya mwezi wa Aprili na Julai 1994.
Paul Kagame alikuwa na umri wa miaka 36 pekee wakati chama chake, Rwandan Patriotic Front (RPF), kilipowaondoa Wahutu wenye msimamo mkali kutoka madarakani, wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ambayo yaligharimu maisha ya watu 800,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hasa Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani, kati ya mwezi wa Aprili na Julai 1994. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

"Katika nchi nzima, tarehe ya kuchaguliwa kwa rais wa Jamhuri na wabunge 53 kutoka kwa orodha iliyopendekezwa na mashirika ya kisiasa au kwa wagombea huru ni Julai 15, 2024," Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi imetangaza kwenye X ( zamani ikiitwa Twitter). Wagombea wataweza kufanya kampeni kuanzia Juni 22 hadi Julai 12, tume hiyo imeongeza.

Mnamo mwezi Machi, serikali ilitangaza kuwa uchaguzi wa urais na wa wabunge utafanyika siku hiyo hiyo. Paul Kagame, 66, alitangaza kuwania muhula wa nne mwezi Septemba. Alifanya marekebisho ya katiba yenye utata ambayo yalimuwezesha kuwania muhula wa tatu na yanaweza kumruhusu kutawala hadi mwaka wa 2034.

Kiongozi wa zamani wa waasi, Paul Kagame amekuwa kiongozi mkuu wa nchi katika eneo la Maziwa Makuu tangu mwisho wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994. Aliongezwa muhula kusalia madarakani - kwa zaidi ya 90% ya kura - katika uchaguzi wa mwaka 2003, 2010 na 2017. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Green Party, Frank Habineza, pia alitangaza kuwania 2024.

Rwanda inajionyesha kama moja ya nchi tulivu zaidi katika bara la Afrika, lakini mashirika kadhaa ya haki za binadamu yanamshutumu Paul Kagame kwa kutawala katika mazingira ya hofu, kukandamiza upinzani na uhuru wa kujieleza.

Kagame alikuwa na umri wa miaka 36 pekee wakati chama chake, Rwandan Patriotic Front (RPF), kilipowaondoa Wahutu wenye msimamo mkali kutoka madarakani, wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya halaiki ambayo yaligharimu maisha ya watu 800,000 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hasa Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani, kati ya mwezi wa Aprili na Julai 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.