Pata taarifa kuu

Marekani imezitaka Rwanda na DRC kuepusha mzozo unaoweza kutokea baina ya nchi hizo

Nairobi – Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, hapo jana ameripotiwa kuzungumza kwa nyakati tofauti na rais wa DRC, Felix Tshisekedi pamoja na mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, ambapo amewataka kuepusha mzozo unaoweza kutokea baina ya nchi hizo.

Katika mazungumzo yake na viongozi hao, amejadiliana não kuhusu hali ya usalama kwenye êneo la mashariki mwa DRC
Katika mazungumzo yake na viongozi hao, amejadiliana não kuhusu hali ya usalama kwenye êneo la mashariki mwa DRC AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Katika mazungumzo yake na viongozi hao, amejadiliana não kuhusu hali ya usalama kwenye êneo la mashariki mwa DRC na umuhimu wa nchi hizo mbili kushirikiana katika masuala ya usalama.

Aidha Blinken, amewataka viongozi hao, kila mmoja kuwaondoa wanajeshi Wake kwenye maeneo ya mpakani, kama moja ya njia ya kupunguza mvutano baina ya mataifa hayo mawili.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani amesemekana kufanya mazungumzo na viongozi hao kwa njia ya simu
Mwanadiplomasia huyo wa Marekani amesemekana kufanya mazungumzo na viongozi hao kwa njia ya simu REUTERS - ELIZABETH FRANTZ

Simu ya Blinken na viongozi hao, imekuja wakati ambapo mvutano baina ya nchi hizo mbili ukishika kasi, Kinshasa ikiituhumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi wa M23 kutatiza usalama mashariki mwa nchi hiyo pamoja na kuingia wanajeshi Wake.

Hata hivyo Rwanda licha ya kuendelea kukanusha madai hayo, inasema DRC imekuwa ikishirikiana na makundi ya waasi kutaka kutatiza usalama wake, ikilitaja moja kwa moja kundi la waasi wa zamani wa Rwanda, FDLR.

DRC imekuwa ikiituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 suala ambalo kigali imeendelea kukana
DRC imekuwa ikiituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 suala ambalo kigali imeendelea kukana © AFP - SIMON WOHLFAHRT

Hii si mara ya Kwanza kwa Blinken, kuzungumza kwa simu na viongozi hawa, ambapo licha ya yeye mwenyewe miezi kadhaa nyuma kufanya ziara kwenye nchi hizo, amekuwa aksisitiza umuhimu wa mataifa hayo kujiepusha na mivutano aliyosema inatishia usalama wa ukanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.