Pata taarifa kuu

Rais wa Ujerumani Waiter Steinmeier anazuru nchini Tanzania

Rais wa Ujerumani Frank Waiter Steinmeier yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu, pamoja na kuzungumza na mwenyeji wake Samia Suluhu Hassan kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia na kimaendeleo katika sekta mbalimbali.

Rais wa Ujerumani anazuru nchini Tanzania, mataifa hayo yakilenga kuimarisha ushirikiano
Rais wa Ujerumani anazuru nchini Tanzania, mataifa hayo yakilenga kuimarisha ushirikiano AP - Petros Giannakouris
Matangazo ya kibiashara

Rais Steinmeier aliwasili kwenye taifa hilo akiwa ameambatana na viongozi wengine wa serikali pamoja na wawekezaji wa kampuni kutoka ujerumani.

Akiwa nchini Tanzania, Steinmeier watajadili na mwenyeji wake, rais Samia Suluhu Hassan katika Ikulu jijini humo namna ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na kimaendeleo uliodumu kwa zaidi ya miaka 60.

Marais hao watashiriki jukwaa la kibiashara linalohusisha wafanyabiashara wa nchi hizo, thamani ya bidhaa kutoka Ujerumani ni Dola za kimarekani Milioni 42 huku zinazoingia Tanzania zikifia thamani ya Dola Milioni 237.

Ziara hii inakuja wakati huu ambapo Urusi imesitisha usafirishaji wa gesi katika mataifa ya Ulaya, kufuatia vita na Ukraine hivyo ujerumani kama ilivyo kwa mataifa mengine ya Ulaya inasaka washirka wapya barani Afrika huku Tanzania ikiwa miongoni mwa mataifa yenye visima vya gesi.

Rais Steinmeier anatarajiwa kuhitimisha zaira hii kwa kutembelea makumbusho ya vita vya Majimaji, mjini Songea na baadae kuelekea nchini ya Zambia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.