Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier kuzuru Tanzania Jumatatu

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier anatarajiwa kufanya ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Tanzania siku ya Jumatatu Oktoba 29, 2023, kabla ya kuelekea Zambia.

Jumatano Novemba 1, Rais wa Ujerumani atasafiri kuelekea Zambia kwa ziara ya kiserikali.
Jumatano Novemba 1, Rais wa Ujerumani atasafiri kuelekea Zambia kwa ziara ya kiserikali. AP - Czarek Sokolowski
Matangazo ya kibiashara

 

Kwenye ajenda ya ziara yake, rais wa Ujerumani atakutana kwa mazungumzo na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam, ambapo pia atashiriki katika majadiliano na wawakilishi wa wafanyabiashara wa Ujerumani na Tanzania kutazama matarajio ya baadaye ya mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

Rais Frank-Walter Steinmeier atatembelea kiwanda cha saruji kinachoendeshwa na kampuni ya Ujerumani, pia atafanya mkutano na wawakilishi wa vyama vya kiraia vya Tanzania.

Jumanne atasafiri hadi Songea kusini mwa nchi kutembelea makaburi ya waathirika wa vita vya Maji Maji na kuzungumza na vizazi vya waathirika, baada ya kuangazia historia ya Tanzania na hasa utawala wa kikoloni wa Wajerumani. 

Na baadae atazuru Makumbusho ya Kumbukumbu ya Vita vya Maji Maji.

Jumatano Novemba 1, Rais wa Ujerumani atasafiri kuelekea Zambia kwa ziara ya kiserikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.