Pata taarifa kuu

DRC: Baadhi ya wanajeshi wa Afrika Kusini wameamuriwa kurejea nyumbani

Nairobi – Jeshi la Afrika Kusini limewaamuru kurudi nyumbani kwa kundi la wanajeshi wake, wanaotuhumiwa kwa utovu wa nidhamu unaohusiana na unyanyasaji wa kingono nchini DRC, hadi uchunguzi ufanyike.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Afrika Kusini, uzito wa tuhuma zinazowakabili ndio umechangia kuchukua uamuzi wa kuwarudisha nyumbani kwa mahojiano zaidi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Afrika Kusini, uzito wa tuhuma zinazowakabili ndio umechangia kuchukua uamuzi wa kuwarudisha nyumbani kwa mahojiano zaidi AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Wanane hao, ni sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, na walikuwa wanazuiliwa tangu juma lililopita, kwenye kambi yao iliyoko mjini Beni mashariki mwa nchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Afrika Kusini, uzito wa tuhuma zinazowakabili ndio umechangia kuchukua uamuzi wa kuwarudisha nyumbani kwa mahojiano zaidi.

Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu unaohusiana na unyanyasaji wa kingono nchini DRC, hadi uchunguzi ufanyike
Wanajeshi hao wanatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu unaohusiana na unyanyasaji wa kingono nchini DRC, hadi uchunguzi ufanyike © AFP

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema MONUSCO ilipokea ripoti ya wafanyakazi waliohusika na kwamba walishiriki vitendo hivyo baada ya saa za amri ya kutotoka nje, katika baa moja inayojulikana kuwa mahali ambapo wanawake hujiuza.

Aidha jeshi la Afrika kusini limesema halikutaarifiwa mapema kuhusu tuhuma hizo, hadi ilipoona zimechapishwa na vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.