Pata taarifa kuu

DRC : HRW yaeleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea kuzuiliwa kwa Stanis Bujakera

Nairobi – Shirika la kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limeelezea wasiwasi wake kuhusu kuendelea kushikiliwa kwa mwanahabari Stanis Bujakera ambaye sasa anamaliza wiki yake ya tatu akiwa kizuizini.

Awali mahakama ilikataa ombi la kuachiliwa kwa muda lililowasilishwa na mawakili wake
Awali mahakama ilikataa ombi la kuachiliwa kwa muda lililowasilishwa na mawakili wake © Avec l'aimable autorisation de actualite.cd
Matangazo ya kibiashara

Awali mahakama ilikataa ombi la kuachiliwa kwa muda lililowasilishwa na mawakili wake.

Bujakera anashtakiwa kwa kueneza uvumi wa uongo na kusambaza habari za uongo zinazohusisha shirika la ujasusi wa kijeshi kuhusu mauaji ya waziri wa zamani Chérubin Okende.

Thomas Fessy, ni mtafiti aliyebobea wa Human Rights Watch huko DRC, alizungumza na mwenzetu wa RFI Kifaransa Paulina Zidi.

‘‘Hatua ya kukataa ombi la kumwachilia huru Stanis Bujakera kwa muda haiwezi kueleweka na kuendelea kumshikilia kwa muda wa wiki tatau inaonyesha wazi ni mara ngapi anaendelea kuteseka kisaikolojia tangu kukamatwa kwake.’’ alisema Thomas Fessy, ni mtafiti aliyebobea wa Human Rights Watch huko DRC.

00:32

Thomas Fessy, mtafiti aliyebobea wa Human Rights Watch huko DRC

Baada ya kukamatwa kwake katika uwanja wa ndege wa Ndjili wakati akitarajia kwenda mjini Lubumbashi, simu zake na kompyuta ziliripotiwa kuchukuliwa na vyombo vya usalama.  

Mwanahabari huyo ametakiwa na idara ya ujasusi kuweka wazi waliompa taarifa hiyo ambayo mamlaka inasema ni ya uongo.

Aliyekuwa waziri wa zamani Chérubin Okende
Aliyekuwa waziri wa zamani Chérubin Okende AP - Samy Ntumba Shambuyi

Waandishi wa habari nchini DRC wanasema wameghadhabidshwa na kukamatwa kwa mwenzao. Kwa mujibu wa EDMOND IZUBA, msemaji wa muungano wa waandishi wa habari wa Kongo amesema, taarifa iliyochapishwa na Jeune Afrique haina saini yake.

Balozi kadhaa zimeelezea wasiwasi wao kuhusu hali ya mwanahabari huyo wakati huu ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya uchaguzi mkuu unaopangwa kufanyika tarehe 20 Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.