Pata taarifa kuu

EAC inasema kikosi chake huko mashariki ya DRC kimepata mafanikio

Nairobi – Jumuiya ya Afrika Mashariki, imesema kikosi chake kilichoko nchini Jamuhiri ya Kidemokrasia ya Kongo, kimepata mafanikio makubwa katika kurejesha hali ya amani na utulivu mashariki mwa nchi hiyo.

Vikosi hivyo vilitumwa mashariki ya taifa hilo kujaribu kutatua changamoto za kiusalama zinazowakabili raia katika eneo hilo
Vikosi hivyo vilitumwa mashariki ya taifa hilo kujaribu kutatua changamoto za kiusalama zinazowakabili raia katika eneo hilo AP - Ben Curtis
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wa EAC wamekuwa wakiendelea kuwalinda raia kutokana na makundi ya watu wenye silaha mashariki wa DRC kwa ushirikiano na wale wa FARDC.

Vikosi hivyo vilitumwa mashariki ya taifa hilo kujaribu kutatua changamoto za kiusalama zinazowakabili raia katika eneo hilo.

Aidha katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Peter Mathuki, amekanusha madai kuwa kikosi hicho, kimeshindwa katika majukumu yake.

“Kikosi chetu cha Jumuiya kinafanya kazi nzuri mashariki mwa DRC kwa uongozi wa mwenyekiti wa wanachama rais Évariste Ndayishimiye na marais wengine wanashirkiana vyema kuhakikisha kwamba usalama unarejea na tunashirkiana pia na kikosi cha MONUSCO.” alisema Peter Mathuki.

00:32

Katibu Mkuu wa EAC, Peter Mathuki

Haya yanajiri wakati huu tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa nchini DRC, juma hili imetoa ripoti yake inayoonesha kuwa vitendo vya mauaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadalu vimeongezeka maradufu katika nusu ya kwanza yam waka huu.

Akizungumza na wanahabari jijini New York, msemaji wa umoja wa Mataifa, Staphane Dujarric, amesema vitendo hivyo vimekuwa na madhara zaidi kwa raia hasa wa eneo la mashariki.

“Ripoti inathibitisha mashambulio ya makundi yenye silaha yamekuwa na athari kubwa kwa raia na hasa kwenye êneo la Ituri, Kivu kaskazini na kusini. ” alisema Staphane Dujarric.

00:48

Staphane Dujarric, Msemaji wa UN

Aidha kiongozi huyo alisema kuwa katika miezi sita ya mwaka 2023, wastani wa raia tisa waliuawa kila siku mashariki mwa DRC.

Ripoti hii imetolewa wakati huu makundi yenye silaha mashariki mwa nchi hiyo yakiendelea kuua raia licha ya uwepo wa vikosi vya UN na vile vya nchi za ukanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.