Pata taarifa kuu

DR Congo: Michezo ya Francophonie inaanza jiji Kinshasa

Michezo ya nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa, Francophonie toleo la tisa inaanza rasmi hii leo Ijumaa jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, huku wajumbe wakimiminika katika mji huo mkuu, maandalizi ya mwisho yanafanyika huku baadhi ya watakaoshiriki wakionekana kuwa na wasiwasi ambapo wengine wakionyesha kuwa hawatoshiriki licha ya kuwa wamealikwa.

Karibu washiriki elfu tatu watakutana katika jiji hilo kubwa zaidi duniani linalozungumza lugha ya Kifaransa
Karibu washiriki elfu tatu watakutana katika jiji hilo kubwa zaidi duniani linalozungumza lugha ya Kifaransa © D.R.
Matangazo ya kibiashara

Hakika, kulikuwa na baadhi ya nchi zilizoamua kujiondoa, mfano Luxemburg na pia Quebec. Lakini majirani zake, jimbo la New Brunswick, na Canada wapo tayari kama anavyoeleza mkuu wa wajumbe hao, Christiane Roy.   

“Hatungekosa kushiriki mechi hizo. tukio hili la kipekee liko moyoni. Na kwa wajumbe wengine wote tunatazamia kukutana nanyi.” alisema  Christiane Roy.

 

00:08

Christiane Roy kuhusu michezo ya Francophonie

 

Kwa upande wa Ufaransa, licha ya kuwa ujumbe haujakamilika, meneja Daniel Zelinsky yeye anatamani sana kuona michezo hiyo ikianza.   

“Tunakuja kucheza, tunakuja kushinda. Katika mashindano, tunakuja na wanariadha mabingwa wa juu. Tutakuwepo kwenye mashindano mengi ya kisanii ambapo tunatarajia kushinda na sio kuja kushiriki tu. “ alisema Daniel Zelinsky.

 

00:12

Daniel Zelinsky kuhusu michezo ya Francophonie

 

Jumla ya wanachama 36 wa jumuia ya Francophonie watawakilishwa mjini Kinshasa. Na mmoja wa mabalozi wa michezo hiyo, mchezaji wa Ufaransa mwenye asili ya Cameroon, Sarah Anffou hafichi shauku yake.   

“ Kikubwa ni kwamba wapo wachezaji na wasanii ambao tayari wamefika. Na watu wengi wanayo furaha. Tuko Congo, naona ni ajabu kwamba michezo hii inafanyika hapa.” alieleza Sarah Anffou.

 

00:12

Sarah Anffou, Raia wa Cameroon

 

Michezo hiyo ambayo ilipangwa kufanyika mwaka wa 2021, michezo hii ya 9 itafanyika baada ya kuahirishwa mara mbili. Na karibu washiriki elfu tatu watakutana katika jiji hilo kubwa zaidi duniani linalozungumza lugha ya Kifaransa.   

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.