Pata taarifa kuu

Makubaliano kati ya Tanzania na Hungary kuimarisha ushirikiano zaidi

Nairobi – Rais wa Hungary Katalin Novak amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Tanzania, ziara iliyolenga kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Elimu na biashara.

Tanzania na Hungary zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali
Tanzania na Hungary zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali © ikulu ya Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Katika mazungumzo ya faragha, Rais Samia anasema wameteta mengi yakiwemo,kukuza uhusiano katika Demokrasia, Uchumi, Biashara  na Utalii.

“Tumebaini uwepo wa kiwango kidogo cha Biashara na uwekezaji baina yetu ambapo mwaka 2022 Biashara iliyofanyika ni Dola Milioni 4.2 tu, Tumekubaliana kuongeza fursa za kibiashara na kujitangaza zaidi ili wafanyabiashara kutoka Hungary waje zaidi kuwekeza Tanzania katika maeneo ya kimkakati kama katika Nishati Mbadala, Utalii, Tehama, Madini, Uvuvi, Viwanda na Fedha.” alisema rais Samia.

Tanzania na Hungary zimekuwa zikishirikiana katika sekta ya elimu, ambapo nchi ya Hungary imekuwa ikiwafadhili wanafunzi kwenda kusoma elimu ya juu katika ngazi ya shahada ya kwanza, Uzamili na Uzamivu, Rais Katalina Novak anasema sasa wamepasua mbarika.

“Makubaliano ya leo yanatupa fursa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa kitanzania kusoma nchini Hungary kwa gharama zetu lakini leo tumeoiga hatuankubwa zaidi kwa sababu pia wanafunzi wa Hungary watakuja kusoma Tanzania kwa gharama za Tanzania na pia wanaweza kujifunza lugha wakati huo huo kupata elimu ya juu. alieleza rais Novak.

Ziara hii iliyotamatika inafufua ushirikiano uliodorora uliasisiwa mwaka 1980 husu suala la Usawa wa kijinsia Marais wote wawili wakisema wameonyesha dira kwa wanawake wengi.

Steven Mumbi/Dar es Salaam/RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.