Pata taarifa kuu

Vikosi vya SADC haijulikani vitawasili lini DRC

Nairobi – Msikilizaji ni miezi sasa imepita tangu wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC, watangaze kuwa watatuma wanajeshi wao mashariki mwa DRC kusaidia juhudi za kurejesha usalama, hata hivyo hadi sasa haijafahamika ni lini watapelekwa.

Rais wa DRC, Félix Tshisekedi.
Rais wa DRC, Félix Tshisekedi. Sumy Sadurni / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano aliyoyafanya mwishoni mwa juma lililopita, rais Felix Tschisekedi, alisema kutumwa kwa wanajeshi hao kunategemea utayari wa nchi yake pamoja na kuwa na mpango mzuri wa kuratibu vikosi hivyo ikiwemo kupata rasilimali za kiviwezesha.

Mbali na kutokuweka wazi ni lini hasa wanajeshi wa SADC watawasili, rais Tschisekedi amesisitiza utayari wa nchi yake kuwapokea lakini akasema watatumwa katika muda muafaka kulingana na mahitaji.

Aidha kwa sasa rais Tschisekedi, amesema jambo la msingi ni kuhakikisha mapigano yanakoma mashariki mwa nchi hiyo, akigusia mpango unaoendelea wa kuwahamisha katika eneo moja waasi wa M23, akisema ni muhimu kwa raia kurejea kwenye maeneo yao ili waweze kushiriki uchaguzi wa mwezi Desemba kwa amani.

Hata hivyo licha ya kile rais Tshisekedi amesema ni kupiga hatua katika kudhibiti hali ya usalama mashariki mwa nchi hiyo, amekiri suala la usalama kusalia kuwa ni kikwazo kwa Serikali yake kutimiza ahadi alizotoa kwa wananchi, akizikashifu nchi zinazochochea mzozo nchini mwake.

Haya yanajiri wakati huu DRC ikitaka kuondolewa kwa vikosi kadhaa vya kimataifa vikiwemo vile vya MONUSCO, lakini kuna vya kutoka Burundi, Uganda, Malawi, Afrika Kusini na Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.