Pata taarifa kuu

Marekani inasema haitakuwa busara kuwaondoa MONUSCO mashariki mwa DRC

Marekani inasema haitakuwa busara na ni mapema kuwaondoa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kipindi hiki ambacho inasema hali ya usalama haijaimarika hasa katika maeneo ya Mashariki.

Kinshasa ilikuwa imependekeza kuondoka kwa kikosi hicho baada ya Uchaguzi wa mwezi Desemba
Kinshasa ilikuwa imependekeza kuondoka kwa kikosi hicho baada ya Uchaguzi wa mwezi Desemba © ONU
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imetolewa nba naibu Balozi wa Washington Robert Wood, kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao maalum kuhusu hali ya usalama Mashariki mwa DRC.

‘‘Kuzungumzia hali hii ya dharura,DRC  katika ukanda wa maziwa makuu,inahitaji  nia njema ya kisiasa, mazungumzo ya kisiasa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ili kuleta mageuzi hitajika. ‘‘ alisema Robert Wood.

00:33

Robert Wood Kuhusu MONUSCO nchini DRC

Kinshasa ilikuwa imependekeza kuondoka kwa kikosi hicho baada ya Uchaguzi wa mwezi Desemba.

Baadhi ya wakaazi wa DRC wameonekana kutoridhishwa na utendakazi wa MONUSCO na hata kuandaa maandamano kadhaa kushinikiza kuondoka kwa kikosi hicho ambacho kimekuwa katika ardhi yao tangu 1999 ambapo licha ya uwepo wao, visa vya utovu wa usalama vimeendelea kushuhudiwa.

Haya yanajiri wakati huu Rwanda ikiishutumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kutochukua hatua za haraka kukomesha matamshi ya chuki na kibaguzi dhidi ya Wacongamani wenye asili ya Rwanda.

Balozi wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa, Claver Gatete ameliambia Baraza la Usalama ma Umoja wa Mataifa kuwa, matamshi hayo yanatolewa pia shuleni na yanatumiwa kisiasa.

‘‘Kampeni inayolenga Rwanda na ujumbe wa chuki,huenezwa katika shule na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ya Congo kila siku.Kinachosikitisha zaidi ,maofisa wa serikali wa Congo wanaoneza ujumbe huu wakisingizia uzalendo,ili pia kulinda nafasi zao siasani ‘‘ alisema Claver Gatete.

00:36

Claver Gatete kuhusu Rwanda na DRC

Aidha kiongozi huyo ameomba tume ya haki za binadaam kuchunguza makosa haya na kuchukua hatua hitajika ambapo pia juhudi zinahitajika kuongeza nguvu misingi ya kisheria inayoshughulikia ujumbe wa chuki na uwajibikaji kwa watuhumiwa 

DRC kwa muda sasa imekuwa ikiituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 madai ambayo Kigali kwa upande Wake imekanusha na kuitaka Kinshasa kutatua changamoto zake za ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.