Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Shambulio katika shule ya upili nchini Uganda: Raia wasubiri matokeo ya uchunguzi

Polisi wa Uganda walitangaza Jumatatu tarehe 19 Juni kwamba watu wasiopungua 20 wanashikiliwa kufuatia mauaji yaliyotekelezwa mwishoni mwa juma lililopita katika shule ya sekondari karibu na mpaka wa DRC. 

Ndugu na jamaa wanaomboleza Florence Masika na mwanawe Zakayo Masereka, ambao wote waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF walipokuwa wakitoka kwenye mashambulizi ya Jumamosi kwenye Shule ya Sekondari ya Lhubiriha, wakati wa mazishi yao huko Nyabugando, Uganda, Jumapili, Juni 18, 2023.
Ndugu na jamaa wanaomboleza Florence Masika na mwanawe Zakayo Masereka, ambao wote waliuawa na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF walipokuwa wakitoka kwenye mashambulizi ya Jumamosi kwenye Shule ya Sekondari ya Lhubiriha, wakati wa mazishi yao huko Nyabugando, Uganda, Jumapili, Juni 18, 2023. AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

Kundi la kigaidi la ADF linashukiwa kushambulia shule hiyo, kuwachoma moto na kuwauwa watu 42. 

Mamlaka inasema kwamba uchunguzi unaendelea, lakini familia hazifichi kuonyesha mfadhaiko wao na kesi hiyo inazidi kubadilika kisiasa.

Msimamizi na mwalimu mkuu wa shule hiyo ni miongoni mwa watu 20 waliokamatwa, kwa mujibu wa polisi. Mamlaka inasema kuwa inaendelea kulisakama kundi la ADF ambalo liliwateka nyara wanafunzi sita. Vijana ambao waliwasaidia kubeba vyakula vilivyoibiwa.

Hata hivyo, msemaji wa jeshi alihakikisha Jumatatu jioni kwamba eneo la shambulio hilo lilikuwa salama na tulivu. Walakini, raia bado wan mfadhaiko. Wanafunzi wengi wanapendelea kubaki nyumbani badala ya kurudi shule za eneo hilo. Vyombo vya habari vya ndani vinataja kwa mfano shule hii iliyokuwa na wanafunzi zaidi ya 600 na kujikuta ikiwa na wanafunzi takriban thelathini pekee.

Katika kusubiri kutambuliwa kwa waathirika

Wakati huo huo, sherehe za mazishi zinaendelea. Siku ya Jumatatu, polisi ilisema miili 23 imerejeshwa kwa familia. Wawili bado hawajatambuliwa. Majeruhi sita bado wanatibiwa katika hospitali ya Bwera, karibu na shule iliyoshambuliwa, lakini wawili wamehamishwa karibu kilomita 500 kufika Kampala, mji mkuu.

Takriban miili ishirini bado haijarejeshwa kwa familia. Baadhi ya waathiriwa, waliochomwa moto, hawatambuliki na uchunguzi wa DNA unaendelea. Mwanaharakati wa haki za binadamu Wilson Bwambale anaishi Kajwenge, kijiji kilicho na wahanga 12 kati ya 42. Anaeleza kuwa familia tano bado hazijaweza kuwazika watoto wao. "Familia nyingi zina huzuni mkubwa. Akina mama wanalia tu. Pamoja nasi, tunahitaji mila na sherehe za kitamaduni ili kuweza kuomboleza. Bila miili, haiwezekani,” anasema.

Kesi inachukua mkondo wa kisiasa

Baada ya mauaji haya ambayo hayajawahi kutokea kwa zaidi ya miaka 10, wengine wameanza kudai uwajibikaji. Jumanne hii, kikao cha Bunge kilifungua kikao chake kwa kimya cha dakika moja. Spika wa Bunge amezitaka Wizara za Ulinzi na Mambo ya Ndani kuwasilisha ripoti kuhusu maendeleo ya uchunguzi na hatua zilizochukuliwa kufuatia shambulio hilo. Mamlaka imetangaza kuongezeka kwa usalama katika eneo lililoathiriwa. Baadhi ya majengo ya umma sasa yatahitaji zaidi ya walinzi wawili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.