Pata taarifa kuu

DRC : MONUSCO yalaani shambulio la CODECO kwenye kambi ya wakimbizi

NAIROBI – Tume ya umoja wa Mataifa nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeelaani vikali shambulio lililofanywa na waasi CODECO, waliolenga kambi ya wakimbizi ya Lala iliyoko umbali wa kilometa 75 kutoka Bunia, wilayani Djugu jimbo la Ituri, mashariki mwa DRC.

Waasi wa CODECO wametuhumiwa kwa kutekeleza shambulio katika kambi ya wakimbizi mashariki ya DRC
Waasi wa CODECO wametuhumiwa kwa kutekeleza shambulio katika kambi ya wakimbizi mashariki ya DRC AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 45 wameripotiwa kuuawa katika shambulio hilo, ambapo umoja wa Mataifa kupitia msemaji wake Stephen Dujarric, uhalifu huo haukubaliki na wahusika wakamatwe.

‘‘Ujumbe wa amani wa umoja wa mataifa nchini DRC MONUSCO umelaani vikali shambulio ambalo lilitekelezwa Jumatatu usiku katika kambi ya Lala.’’ alisema Stephen Dujarric, msemaji wa UN.

00:34

Stephen Dujarric, msemaji wa UN

Shambulio hili limetekelezwa licha ya operesheni za kijeshi zinazoendelea dhidi ya makundi yenye silaha, mashariki mwa nchi ya DRC, tukio linaloibua maswali zaidi.

Daktari Jean Baptiste DRAJIRO msimamizi wa afya katika jimbo la BULE.

‘‘Tuna pokea watu nane wenye walijeruhiwa kutoka katika kambi ya LALA, tutawatuma jijini BUNIA kwa sababu hatuna vifaa vinavyohitajika kuwasiaidia hapa kwetu.’’ alisema daktariJean Richard DHEDA KONDO, ni kiongozi wa eneo la Bahema Badjere . Jean Baptiste DRAJIRO.

00:24

Daktari Jean Baptiste DRAJIRO msimamizi wa afya katika jimbo la BULE

" Ni waasi wa CODECO ambao walishambulia kambi ya wakimbizi na kisha kuwakata kwa mapanga, kuchoma nyumba zao." alieleza Richard DHEDA KONDO.

00:17

Jean Richard DHEDA KONDO, ni kiongozi wa eneo la Bahema Badjere

Tarehe kumi ya mwezi Juni, raia wengine saba waliuawa wakiwemo watoto watano, katika shambulio ambalo lilitekelezwa na waasi hao wa CODECO, katika wilaya jirani ya Mahagi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.