Pata taarifa kuu

Rwanda: Rais Kagame atekeleza mageuzi katika idara ya jeshi na ujasusi

NAIROBI – Rais wa Rwanda Paul Kagame amewateua wakuu wapya wa kijeshi na wa ujasusi katika mabadiliko makubwa ambayo ameyatekeleza.

Paul Kagame, ametekeleza mageuzi kwenye idara ya jeshi
Paul Kagame, ametekeleza mageuzi kwenye idara ya jeshi REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Rwanda amemteua Juvénal Marizamunda kuhudumu katika nafasi ya waziri wa ulinzi, akichukua nafasi yake Meja  jenerali Albert Murasira, ambaye amekuwa akihudumu katika wadhifa huo tangu mwaka wa 2018.

Mkuu mpya wa majeshi Luteni Jenerali Mubarakh Muganga, anachukua  nafasi yake jenerali Jean Bosco Kazura amabye amekuwa akiongoza jeshi la RDF tangu Novemba mwaka wa 2019.

Mabadiliko kama haya ambayo mkuu wa jeshi na waziri wa uliznzi wanaondolewa kwa wakati mmoja sio rahisi kutokea nchini Rwanda. Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu mabadiliko haya.

Miongoni mwa mabadiliko hayo, Kanali Francis Regis Gatarayiha aliteuliwa kuwa kaimu mkuu wa ujasusi wa kijeshi, huku Jean Bosco Ntibitura akiwa mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa katika Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NISS).

Brigedia Jenerali Evariste Murenzi ameteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la magereza , akichukua nafasi ya Marizamunda.

Meja Jenerali Alex Kagame amechukua wadhifa wa kamanda wa operesheni za kijeshi nchini Msumbiji, wakati Kanali Théodomir Bahizi atahusika na maswala ya vita nchini Msumbiji.

Tangu mwezi wa Julai mwaka 2021, Rwanda imetuma wanajeshi na polisi nchini Msumbiji - kwa ombi la serikali ya nchi hiyo -kupambana dhidi ya watu wenye itikadi kali wanaodai kuwa Waislamu waliokuwa wameteka maeneo mengi ya jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.