Pata taarifa kuu

DRC na China zakubaliana kuanzisha ushirikiano katika masuala ya biashara

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na China, zimekubaliana kuimarisha uhusiano wao na kuanzisha ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji hasa kwenye sekta ya madini.

Rais Felix Tshisekedi wa DRC na mwenyeji wake wa China Xi Jinping
Rais Felix Tshisekedi wa DRC na mwenyeji wake wa China Xi Jinping REUTERS - THOMAS PETER
Matangazo ya kibiashara

Hayo yameafikiwa kati ya rais Tshisekedi na mwenyeji wake Xi Jinping walipokutana leo Ijuma.

Viongozi hao wawili wamekubaliana kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili ili kila mmoja anufaike sawa, kwenye maeneo muhimu hasa biashara.

Tshisekedi ambaye anazuru China kwa mara ya kwanza, ameapa kujadili upya mikataba ya uchimbaji madini, iliyosainiwa na serikali iliyopita kuhusu namna wawekezaji wa China wanavyowekeza katika sekta ya madini katika nchi yake.

Afisa wa juu wa serikali ya DRC Erik Nyindu Kibambe, aliyeambatana na rais Tshisekedi katika ziara hiyo, amesema mazugumzo kuhusu mikataba ya uwekezaji katika sekta ya madini, yanaendelea vema na yatakuwa na matokeo chanya.

Kiongozi huyo wa DRC atakuwa nchini China hadi Jumatatu ijayo, na mbali na masuala ya biashara na uchumi, Tshisekedi anajadiliana na viongozi wa China pia namna ya ushirikiano kwenye masuala ya siasa na usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.