Pata taarifa kuu

IMF na Kenya wafikia makubaliano ya mkopo wa dola bilioni 1

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limetangaza kwamba limefikia makubaliano ya mkopo wa dola bilioni moja (sawa na euro bilioni 927) kwa Kenya, nchi ya Afrika Mashariki inayokabiliwa na matatizo ya ukwasi na matatizo ya kiuchumi.

Makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, Aprili 8, 2019.
Makao makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Washington, Aprili 8, 2019. REUTERS/Yuri Gripas/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Uchumi wa Kenya umelemewa na deni ambalo linafikia kilele cha dola bilioni 70 (sawa na euro bilioni 65) na kushuka kwa thamani kwa sarafu yake, shilingi, dhidi ya dola.

Katika kujaribu kupunguza deni lake, serikali ya Rais William Ruto imetayarisha bajeti ikijumuisha ushuru mwingi mpya unaopaswa kuleta shilingi bilioni 289 (sawa na euro bilioni 2), ili kukamilisha bajeti kwa shilingi bilioni 3.600 (sawa na euro bilioni 24) iliyopangwa kwa 2023-24.

Mkataba huu bado unahitaji kuidhinishwa na bodi ya wakurugenzi ya IMF, ambayo inakutana mwezi Julai. Iwapo itaidhinishwa, Kenya itakuwa na uwezo wa kufikia dola milioni 410 mara moja, kulingana na IMF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.