Pata taarifa kuu

DRC: Raia waliokimbia makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa waanza kurejea

NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, raia wa Wilaya ya Irumu, mkoani Ituri, kwa kuhofia ya mashambulio ya kundi la ADF na kukimbia katika vijiji vyao vya Bahema Boga, Mitego na  Banyari Tchabi, wameanza kurejea nyumbani. 

Maelfu ya raia wa DR Congo wametoroka makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa na makundi ya waasi
Maelfu ya raia wa DR Congo wametoroka makazi yao kwa hofu ya kushambuliwa na makundi ya waasi © BADRU KATUMBA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kambi za wakimbizi hao zimesalia tupu, baada ya kuondoka kwa raia hao ambao wameanza kurejelea maisha yao ya kawaida. 

Mafanikio haya yanaelezwa kuchangiwa pakubwa kutokana na operesheni ambazo zimekuwa zikiongozwa na kundi la wanajeshi wa Uganda dhidi ya waasi wa ADF kwa kipindi cha siku kadhaa zilizopita. 

Kwa karibu miaka miwili, raia wa êneo la Irumu wamekuwa wakiishi katika kambi iliyo karibu na kambi ya jeshi la Umoja wa Mataifa, MONUSCO. 

Raia wengine, walikimbilia katika vijiji vya Walendu Bindi, baada ya kuongezeka kwa mashambulio ya waasi wa ADF ambayo yamekuwa yakisababisha mauaji. 

Askofu wa Kanisa Angilikana Dayosisi ya Boga, William Bahemuka Mugenyi, amesema kwa karibu miezi miwili sasa, kumekuwa na utulivu katika êneo hilo na asilimia 80 ya wakaazi wa kijiji cha Bahema Boga wamerjea katika ardhi zao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.