Pata taarifa kuu

Kenya yapokea msaada wa ngano kutoka Ukraine

NAIROBI – Nchi ya Kenya, imepokea msaada wa wa tani elfu 30 za ngano kutoka Ukraine, shehena hiyo ikipokelewa na maafisa wa serikali katika bandari ya Mombasa, ikitokea kwenye bandari ya Oddesa kwa lengo la kusaidia taifa hilo kupambana na baa la njaa.

Nchi ya Kenya, imepokea msaada wa wa tani elfu 30 za ngano kutoka Ukraine
Nchi ya Kenya, imepokea msaada wa wa tani elfu 30 za ngano kutoka Ukraine © Gideon Maundu / AP
Matangazo ya kibiashara

Christopher Fomunyoh, ni Mkuregenzi wa Afrika kutoka kituo cha National Democratic Institute huko Washington nchini Marekani, anazungimzia kuwasili kwa msaada huu.

“Meli iliyowasili ina tani elfu 25 ya ngano kutoka Ukraine chini ya mpango wa nafaka wa Black Sea uliotiwa saini tangu mwaka wa 2022.”amesema Christopher Fomunyoh.

Hali ya Ukame unaoshuhudiwa maeneo ya Pembe ya Afrika unaweza kusababisha vifo vya raia 135 kwa siku nchini Somalia kati ya Januari na Juni mwaka huu kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO na UNICEF.

Mapema mwezi huu, WHO lilionya kuwa takriban watu 100,000 nchini Somalia wanakabiliwa na janga la njaa kutokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kukumba eneo hilo katika miongo minne.

Takwimu zinaeleza kuwa kati ya watu 18,100 na 34,200 wanaweza kufa kutokana na atahri za  ukame nchini Somalia katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu.

Hali mbaya ya hewa ikielezwa kusababisha vifo vingine vya watu 43,000 mwaka jana ikilinganishwa na ukame wa mwaka wa 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.