Pata taarifa kuu

Burundi imetangaza mlipuko wa Polio: WHO

NAIROBI – Nchi ya Burundi, imetangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa Polio, baada ya kurekodi mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo katika kipindi cha zaidi ya miongo mitatu, imesema taarifa ya shirika la afya duniani, WHO

Shirika la afya duniani WHO
Shirika la afya duniani WHO AP - Martial Trezzina
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, WHO inasema taifa hilo la Afrika ya Mashariki, lilirekodi wagonjwa 8 wenye maambukizo ya aina ya pili ya virusi vya Polio, ambapo kwa mujibu wa wizara ya afya nchini humo, mgonjwa mmoja ni mtoto wa miaka minne ambaye hakuwa amepata chanjo na wengine wawili ni waliogusana nae.

Virusi vya Polio ni miongoni mwa ugonjwa hatari unaoambukiza, ambapo vimelea vyake hushambulia mfumo wa fahamu na madhara yake huweza kumfanya mgonjwa akapooza.

Wataalamu wa afya wanasema aghalabu ugonjwa huu huwapata watoto, lakini unaweza kuzuiwa kwa chanjo ambazo zinapatikana kwa urahisi ,na sio gharama.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, Mashidiso Moeti, amenukuliwa akisema kuwa kitendo cha mamlaka za Burundi kugundua ugonjwa huu, kunadhhirisha namna taifa hilo limejipanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.