Pata taarifa kuu

DRC: Papa Francis alaani 'ukoloni wa kiuchumi' unaoikabili Afrika

Kiongozi wa kanisa Katolika duniani, Papa Francis, amewasili Jumanne, Januari 31 mapema mchana, katika uwanja wa ndege wa Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Papa yuko nchini humo kwa ziara ya siku nne, kabla ya kuelekea Sudan Kusini. Katika hotuba yake ya kwanza, papa ameshutumu "ukoloni wa kiuchumi" ambao 'unaoikabili' Afrika.

Papa Francis akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi wakati wa hotuba yake ya kwanza katika ikulu ya rais, "Palais de la Nation" mjini Kinshasa, Januari 31, 2023.
Papa Francis akiwa na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi wakati wa hotuba yake ya kwanza katika ikulu ya rais, "Palais de la Nation" mjini Kinshasa, Januari 31, 2023. AFP - TIZIANA FABI
Matangazo ya kibiashara

Francis, akitabasamu, kwenye lami ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo: hizi ni picha za kwanza za ziara ya papa nchini DRC inayoanza Jumanne hii, Januari 31 na inatarajiwa kudumu kwa siku nne. Ndege yake, iliyoondoka Jumanne asubuhi kutoka Roma, ilitua muda mfupi baada ya saa 3:30 alaasiri kwa saa za huko Kinshasa. Wakati ndege hiyo ikishuka, Papa akiwa kwenye kiti cha magurudumu kutokana na matatizo ya kiafya, alilakiwa na Waziri Mkuu wa Kongo Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge.

Umati wa watu ulianza kukusanyika asubuhi karibu na uwanja wa ndege kusherehekea kuwasili kwa kiongozi wa kanisa Katolika duniani. Baada ya sherehe ya kukaribishwa katika uwanja wa ndege, Papa Francis alikwenda ikulu ya rais, "Palais de la Nation", katika mji mkuu wa Kongo, na kupokelewa na Rais Félix Tshisekedi.

"Ondoeni mikono yenu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ondoeni mikono yenu Afrika! "

Katika hotuba yake yenye mtazamo wa kisiasa mbele ya mamlaka na wanadiplomasia, Papa Francis ameshutumu kwa nguvu kile alichokiita "ukoloni wa kiuchumi" ambao "umekithiri" barani Afrika na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini.

"Baada ya ukoloni wa kisiasa, ukoloni wa kiuchumi unaofanya utumwa kwa usawa umekithiri. Nchi hii, ambayo kwa kiasi kikubwa imeporwa, kwa hivyo inashindwa kuchukua fursa ya kutosha ya rasilimali zake kubwa, "Papa Francis amelalamika, huku akipigiwa makofi, wakati wa hotuba yake yenye mtazamo wa kisiasa mbele ya mamlaka na mabalozi wanaowakilish nchi zao nchini DRC.

  "Ondoeni mikono yenu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ondoeni mikono yenu Afrika! Acheni kuikomesha Afrika: si mgodi wa kuchimbwa wala si ardhi ya kuporwa”, amesema Papa Francis na kupigiwa makofi, mbele ya mamlaka na maofisa wa kidiplomasia katika ikulu ya rais.

Wito unaosikika hasa katika nchi yenye utajiri mkubwa na ardhi yenye rutuba, ambapo thuluthi mbili ya wakazi takriban milioni 100 wanaishi chini ya dola 2.15 kwa siku.

“Hatuwezi kuzoea damu ambayo imekuwa ikitiririka kwa miongo kadhaa nchini DRC, na kusababisha mamilioni ya vifo. Naomba michakato inayoendelea ya amani - ambayo ninahimiza kwa nguvu zangu zote - iungwe mkono kivitendo na kwamba ahadi zitekelezwe," papa pia ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Jumanne jioni, maelfu ya watu wanatarajiwa kukusanyika katika uwanja wa ndege wa Ndolo kwa ajili ya mkesha wa maombi kabla ya misa ya Jumatano asubuhi. Waumini milioni moja wanatarajiwa kuhudhuria misa hiyo.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.