Pata taarifa kuu
DRC

Watu 12 wauawa, washambuliwa na watu wenye silaha nchini DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watoto watano ni miongoni mwa watu 12 waliouawa siku ya Ijumaa , Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya kushambuliwa na kundi moja la waasi, ambalo halikushiriki kwenye mazungumzo yaliyofanyika jijini Nairobi.

Wakaazi wa Kivu Kaskazini waliokimbia makwao kwa sababu ya mashambulio ya mara kwa mara
Wakaazi wa Kivu Kaskazini waliokimbia makwao kwa sababu ya mashambulio ya mara kwa mara © badru Katumba / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha Walendu Watsi, ambako wakaazi walikatwa kwa mapanga na wengine kuteketezwa hadi kufa, kwa mujibu wa viongozi wa eneo hilo.

Ripoti zinasema, watu waliolengwa ni kutoka kabila la Lendu kwa mujibu wa msemaji wa kabila hilo Jean-Marie Ndjaza.

Katika hatua nyingine, mapigano mapya yalizuka hapo jana kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali ya DRC, ripoti zikielezea kuwa, yameendelea mpaka leo, Wilayani Rutshuru baada ya kuanzia Bwiza eneo ambalo limekuwa likidhibitiwa na waasi hao.

Mapigano haya yamekuja siku 10 baada ya kushuhudiwa kwa utulivu na waasi hao kukutana na maafisa wa Jeshi la DRC na wadau wengine, huko Kibumba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.