Pata taarifa kuu
SUDAN KUSINI-AU

AU kujadili hatima ya kuundwa kwa Mahakama maalum Sudan Kusini

Tume ya Umoja wa Afrika inayoshughulikia masuala ya usalama na amani inakutana leo kujadili vita ambavo vimekuwa vikiendelea nchini Sudan Kusini tangu mwak 2013 na kusababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Viongozi wa Sudan Kusini  Salva Kiir (Kushoto), ana Makamu wa kwanza wa rais  Riek Machar katika kikao cha pamoja
Viongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir (Kushoto), ana Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar katika kikao cha pamoja AFP - PETER LOUIS GUME
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja siku chache baada ya Shirika la Kimataifa la Kutetea haki za binadamu la Amnesty International na mashirika mengine ya kirai nchini Sudan Kusini, kuishinikiza Umoja wa Afrika kuunda kwa haraka Mahakama maalum kuchunguza visa hivyo.

Katika mkataba wa amani wa Sudan Kusini wa mwaka 2015 na 2018 ilikubaliwa kuwa Mahakama hiyo iundwe lakini mpaka leo, hilo halijafanyika, huku watuhumiwa wa kijeshi na siasa wakiendelea kuwa huru.

Wanaharakati nchini Sudan Kusini wanasema, Mahakama hiyo haijaundwa kwa sababu hakuna utashi wa kisiasa, ili kuundwa kwa Mahakama hiyo kwa sababu wanasiasa wenyewe ndio wahusika wakuu wa mateso ya raia.

Tume hiyo ya Umoja wa Afrika inapokutana, wanaharakati wanatumai kuwa Sudan Kusini itashinikizwa kuunda Mahakama hiyo, itakayokuwa chini ya Umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.