Pata taarifa kuu

Kenya: Utulivu wakati matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa Jumanne

Kulingana na Katiba ya nchi matokeo ya Uchaguzi wa urais yanatarajiwa kutangazwa kwa muda wowote hadi kesho Jumanne. Hata hivyo baadhi ya wakazi katika maeneo ya Kisumu na Eldoret wamefurika barabarani kuanza kusherehekea, huku wakitaka mshindi kutangazwa.

Kenya, Nairobi, Agosti 13, 2022: Tume ya Uchaguzi ikifanya kazi kwa bidii katika Kituo cha Bomas, ikijumlisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Kenya, Nairobi, Agosti 13, 2022: Tume ya Uchaguzi ikifanya kazi kwa bidii katika Kituo cha Bomas, ikijumlisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Jumapili jioni, tume ya uchaguzi ilivuka kizingiti cha maeneo 200 ya bunge (kati ya 292) ambayo matokeo yake yalichunguzwa na kuthibitishwa. Baada ya wikendi yenye mvutano, iliyoambatana na mzozo kati ya wafuasi wa wagombea wawili wakuu ndani ya kituo kikuu cha kujumlisha kura, wito wa utulivu na uvumilivu umeendelea kutolewa.

Polisi wa kutuliza ghasia, vikosi maalum... usalama katika kituo cha kukusanya matokeo umeimarishwa zaidi tangu Jumapili.

Katika mazingira hayo ya mvutano, mashirika 14 yasiyo ya kiserikali, mashirika ya kiraia na vyama vya wafanyakazi vimeungana kuomba utulivu na uvumilivu, wakati Tume ya Uchaguzi ikikamilisha kazi yake. “Tunatoa wito kwa wagombea wote wa kisiasa na wafuasi wao kuruhusu mchakato huu kufanyika kikatiba hadi tamati yake,” amesema Mwaura Kabata, mmpoja wa wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Kenya. Wahusika wote waliodhulumiwa watakuwa na haki ya kwenda mahakamani na kutafuta suluhu ya kisheria.”

Kwa sababu kila muungano kati ya miungano miwili inayopinga uchaguzi huu wamekuwa wakiwaambia wafuasi wao kwamba wamepata ushindi. Hotuba za chuki zimekuwa zikitolewa, ameonya Khalid Hussein kutoka shirika lisilo la kiserikali la HAKI AFRICA. “Mtazamo wa wanasiasa hutukatisha tamaa. Kupiga mabomu kifuani haimaanishi chochote kwa kuboresha hali hiyo. Kwa hivyo tunatoa wito kwa Wakenya kutoyumbishwa na maneno haya ya ushawishi. Hata matokeo yaweje, tuwe tayari kuyakubali na kuendelea kuishi pamoja. "

Tume ya uchaguzi inatarajiwa kumtangaza rais mteule leo. Tume hiyo ina siku hadi saba za kutangaza matokeo baada ya uchaguzi kufanyika. Uchaguzi mkuu wa Kenya ulifanyika Jumanne wiki iliyopita tarehe 9 Agosti.

Iwapo mshindi wa urais atatangazwa leo,na iwapo hapatakuwa na pingamizi ya ushindi wake mshindi anafaa kuapishwa tarehe 30 mwezi huu wa Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.