Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini Kenya: Mvutano waibuka katika Tume ya Uchaguzi

Mvutano umeongezeka nchini Kenya, siku tano baada ya uchaguzi wya urais. Matokeo bado yanakusanywa na kuthibitishwa na Tume ya Uchaguzi. Tuya Uchaguzi ina hadi siku ya Jumanne, Agosti 16 kutangaza matokeo ya uchaguzi. Hata hivyo, kadri watu wanavyosubiri, ndivyo hasira inavyozidi kuongezeka. Shutuma za kujaribu kuiba kura zinaongezeka, kama vile wito kwa utulivu.

Moja ya vituo vyaa kupigia kura nchini Kenya, Agosti 9, 2022.
Moja ya vituo vyaa kupigia kura nchini Kenya, Agosti 9, 2022. © RFI/Laura-Angela Bagnetto
Matangazo ya kibiashara

Dalili ya kuongezeka kwa mvutano huo, polisi wa kutuliza ghasia waliingilia kati jana usiku huko Bomas of Kenya, ambapo Tume ya Uchaguzi ya Kenya imweka kituo chake cha kitaifa cha kuhesabu kura.

Tangu jana Jumamosi Agosti 13, wawakilishi wa wagombea mbalimbali wanaoshiriki katika uhakiki wa kura hizo walinusurika kupigwa, mara kadhaa. Kulikuwa na visa vya mapigano dhidi ya shutuma za pande zote za kujaribu kuiba kura, hadi karibu wakati ambapo mmoja wa wawakilishi wa Raila Odinga alipanda jukwaani na kutangaza: "Ninataka kuwaambia Wakenya kwamba Bomas ni eneo la uhalifu," aliyazungumza hayo wakati matangazo yalikuwa yakirushwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Jumapili hii asubuhi, utulivu umerejea pamoja na zoezi la kuhesabu matokeo. Idadi ya maafisa wa usalama na vikosi vya ulizi  imeongezwa.

Katika hali hii, takriban vyama kumi na tano nchini Kenya, miungano na mashirika yasiyo ya kiserikali yametoa wito wa utulivu Jumapili asubuhi. “Tumesikitishwa na tabia ya wanasiasa. Katika kila uchaguzi kuna mshindi na mshindwa,” wamesema huku wakiwataka wafuasi wa pande zote mbili kujizuia hadi tume ya uchaguzi itakapomaliza kazi yake.

Wakati huo huo, katika ishara ya kutoa wito kwa utulivu, Raila Odinga amezungumza leo asubuhi kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa urais, wakati wa ibada ya Jumapili huko Karen. “Tunatumai kuwa amani itakuwepo baada ya uchaguzi. Sisi sote ni sehemu ya taifa moja,” amesema.

William Ruto, ambaye pia alihudhuria misa leo asubuhi, hakutoa tamko lolote.

Mgombea David Mwaure, wa chama cha Agano, amekubali kushindwa. Amepata chini ya 1% ya kura, kulingana na makadirio ya awali. Wagombea wanne walikuwa kwenye kinyang'anyiro hicho lakini sasa kila kitu kimeamuliwa kwa mchuano mkali kati ya wawili wanaochuana vikali, Raila Odinga na William Ruto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.