Pata taarifa kuu

Uchaguzi Kenya: Hali ya wasiwasi yaongezeka kwa kusubiri matokeo

Siku tatu baada ya Uchaguzi Mkuu, Wakenya bado wanasubiri kwa hamu jina la mshindi wa uchaguzi wa urais. Mashaka ambayo husababisha hofu kati ya raia.

Wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa na wawakilishi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura cha IEBC, Bomas of Kenya, Nairobi, Kenya mnamo Agosti 11, 2022.
Wajumbe kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa na wawakilishi wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika kituo cha kitaifa cha kuhesabu kura cha IEBC, Bomas of Kenya, Nairobi, Kenya mnamo Agosti 11, 2022. REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi umekuwa ukiendelea nchini Kenya tangu zoezi la kupiga kura Jumanne tarehe 9 Agosti. Kazi ni kubwa itachukuwa siku nyingi kwa Tume ya Uchaguzi, ambayo inapaswa kuangalia ripoti zote zinazotumwa na vituo vya kupigia kura. Kwa ajili ya uwazi, IEBC inaweka matokeo hayo mtandaoni saa baada ya saa. Vyombo vya habari vinachukua fursa hiyo kuonyesha, tangu Jumanne jioni, idadi yao ya kura, lakini wakati mwingine hupingana.

Akitangaza matokeo ya mwanzo mwanzo kutoka maeneo bunge, Chebukati alisisitiza kuwa kauli ya mwisho ni ya IEBC.

Amesema ”shughuli ya kumtangaza mshindi ni kazi ya tume ya IEBC. Mawakala wanaweza kujumlisha matokeo yao ila kauli ya mwisho ni ya tume ya uchaguzi.”

Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, IEBC inapewa wiki moja tangu siku ya kupigwa kura, iwe imeshakamilisha utangazaji matokeo. Kwa hivyo, mwisho ya kumtangaza mshindi wa urais ni 16 Agosti ambayo ni siku saba baada ya uchaguzi mkuu kufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.