Rwanda: Balozi wa Uingereza akana barua inayokosoa mpango wa Rwanda na Uingereza
Balozi wa Uingereza nchini Rwanda, Omar Daair, amekana kuandika barua iliotumwa kwa afisi ya mambo ya nje ya Uingereza, ikishauri Uingereza kusitisha mpango wake wa kuhamishia wahamiaji nchini Rwanda.
Imechapishwa:
Barua hiyo inatuhumu serikali ya Rwanda kwa kuwa na história inayokandamiza haki za biandamu, kwa mjibu wa stakabadhi zilizowasilishwa mahakamani na wale wanaopinga mpango kati ya Rwanda na Uingereza
Balozi Daair, amesema barua hiyo aliandikwa na mtangulizi wake, miezi miwili kabla yake kuanza rasmi majukumu yake.
Mpango wa Rwanda na Uingereza kuwahamisha wahamiaji hadi nchini Rwanda umepingwa vikali na mashariki ya kutetea haki za binadamu kesi ikiwasilishwa mahakamani.