Pata taarifa kuu
Msumbiji - Usalama

SADC: Yaongeza muda wa wanajeshi wake kuhudumu Musumbiji

Mataifa ya kusini mwa Africa , Sadc, yamekubaliana kuongeza muda wa wanajeshi wake kuendelea kuhudumu nchini Musumbiji kwa kipindi cha mwezi moja kuendelea kupambana na wanajihadi.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa Msumbiji Filipe Nyusi (kulia) wakizungumza wakiwa wamevalia sare za kijeshi mbele ya wanajeshi wao huko Pemba, Septemba 24, 2021,  Cabo Delgado.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na mwenzake wa Msumbiji Filipe Nyusi (kulia) wakizungumza wakiwa wamevalia sare za kijeshi mbele ya wanajeshi wao huko Pemba, Septemba 24, 2021, Cabo Delgado. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inajiri wakati huu wanajihadi, wakianzisha tena mashambilizi kaskazini mwa taifa hilo.

Uvamizi ukienea katika miji ya Niassa na Nampula, mamlaka eneo hilo zikitilia hofu idadi kubwa ya vijana wanaosajiliwa kujiunga na makundi ya kijihadi.

Zaidi ya raia 800,000 wamekimbia makwao tangu mashambulizi kuanza miaka tano iliopita.

Mkowa wa Cabo Delgado ni ngome ya wapiganaji wenye uhusiano na kundi la Islamic State.

Wanajeshi wa Rwanda pia wapo nchini Musumbuji kupambana na wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.