Pata taarifa kuu
MUSUMBIJI - USALMA

Musumbiji – Mashambulizi ya wanajihadi yaathiri pakubwa watoto kisaikolojia

Shirika la kimataifa la kutetea haki za watoto, la Save the Children,  katika ripoti yake limesema watoto nchini Musumbuji wameathirika kisaikolojia kutokana na visa vya mashambulizi ya wanajihadi, hasa katika mkowa wa Cabo Delgado.

Watoto katika mkowa wa  Cabo Delgado, nchini Musumbji.
Watoto katika mkowa wa Cabo Delgado, nchini Musumbji. © Liliana Henriques / RFI
Matangazo ya kibiashara

Save the Children, limesema baadhi ya watoto walishuhudia wazazi wao wakiuawa na wajihadi na hilo limeathiri pakubwa hali yao kiafya.

Ripoti hiyo inazidi kueleza  kufikia sasa zaidi ya watoto millioni moja wamekimbia makwao kutokana na vurugu zilizoanza mwaka 2017 nchini Musumbiji.

Save the Children, linasema tabia za watoto hubadilika kila mara na kwamba huenda watoto wakakosa kusahau matukio hayo, hadi pale watakapopewa matibabu ya akili.

Kundi la wanajihadi linalofahamika na wenyeji wa cabo Delgado kama al-Shabaab limekuwa likitekeleza mashambulizi eneo hilo.

Mwezi machi mwaka huu wapiganaji hao waliuteka mji wa Palma ambao upo karibu na sehemu kunakochimbwa madini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.