Pata taarifa kuu

Mfalme wa Ubelgiji atamatisha ziara yake DRC

Mfalme Philippe wa Ubelgiji, ametamatisha ziara yake nchini DRC kwa kutembelea mjini Bukavu, Mashariki mwa nchi hiyo, alikokutana na wanawake waliobakwa na kunyanyaswa kimapenzi kufuatia utovu wa usalama katika eneo hilo.

Mfalme Philippe wa Ubelgiji (wa pili kushoto) akimsikiliza daktari Denis Mukwege (kulia) aliyewasilisha timu yake katika hospitali ya Panzi huko Bukavu, Juni 12, 2022.
Mfalme Philippe wa Ubelgiji (wa pili kushoto) akimsikiliza daktari Denis Mukwege (kulia) aliyewasilisha timu yake katika hospitali ya Panzi huko Bukavu, Juni 12, 2022. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa hotuba yake mbele ya Mfalme Philippe akiwepo pia Waziri Mkuu wa DRC Sama Lukonde, Daktari Denis Mukwege alikashifu kutokuadhibiwa kwa uhalifu uliofanywa kwa miaka mingi nchini Congo:

Ni kukosa kuadhibiwa wahalifu raia wa Congo na wa kigeni ndio inachochea ghasia katika eneo hili na mashambulizi mengi ambayo nchi yetu inakabilina nayo. Shambulizi la hivi punde ni lile la kundi la M23, ambalo linaungwa mkono na Rwanda.

Waziri wa Ushirikiano wa Ubelgiji Meryame Kitir anatambua haki ya DRC kutetea ardhi yake na raia wake, lakini anatoa wito kwa utulivu:

DRC na majirani zake lazima wazidishe juhudi za ndani kuboresha hali ya usalama. Kuanzishwa mchakato wa kidiplomasia katika kanda hii ili kurejesha imani na utulivu inaonekana kuwa na uharaka kwetu.

Vumilia Kabubu ni miongoni mwa wanawake wahanga waliohudumiwa kwenye hospitali ya Panzi :

Kilicho kuwa muhimu wajikaze wakubaliane kumaluiza vita hivi, na pia bado kuna visa vya ubakaji”

Waziri wa Ushirikiano wa Ubelgiji anahofia kwamba ghasia za sasa zinaweza kuhatarisha kuongezeka kwa idadi ya waathiiriwa kati ya raia katika mkoa huo. Mfalme Philippe anatarajia kuondoka DRC leo Jumatatu Juni 13, 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.