Pata taarifa kuu
Kenya - Afya

Kenya yashuhudia ukosefu wa mipira ya ngono

Jiji la Kisumu nchini Kenya, wiki hii limeshuhudia uhaba wa mipira ya kondomu, wakati huu mkutano wa majiji-Africities, ukimalizika leo.

Mipira ya kufanya tendo la ndoa
Mipira ya kufanya tendo la ndoa Pixabay
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Afya katika Kaunti ya Kisumu, imethibitisha uhaba wa mipira hiyo, na kuwataka wageni wanaohudhuria mkutano huu kutotegemea kupata mipira ya bure.

Gregory Ganda Kaimu Waziri wa Afya katika Kaunti ya Kisumu.

Kuna ukosefu wa condom katika nchi yote ya Kenya na Kisumu ni Moja ya kaunti hizi zote ,Kisumu ilikuwa na stock yote ambayo ingeweza kupeana lakini sasa kiwango kimeenda chini, kwa saa hizi Jaramogi Hospital peke yake ndio yenye kuwa na Condoms ambazo ziko bure, hospital na maeneo pengine ya umma Condoms zipo zinapeanwa kwa ajili ya planning familial na kulinda raia, na hii itatuliwa Nairobi

 

Erick Okioma, mwanaharakti anayefahamika Kisumu, kuhamasisha umma kuhusu maambukizi ya Ukimwi, hasa mitaani  Kisumu.

Condoms ambazo hazipatikani ni zile Zinazopeanwa bure na serikali na hizo ndio watu wengi katika vitongoji duni watu hutafuta kwa kiasi kikubwa zinatumiwa kwa sababu hizo zinazonunuliwa kwa duka ni shilingi mia chini ya dola moja na hiyo ni shida, na sio kisumu pekeyake

 

Jarid Bolo ni msambazaji wa mipira hiyo ya kondomu, anasema uhaba huu ni jambo la kawaida hasa katika jiji la kisumu ,linapokuwa na wageni au Shule zinapofungwa, na sasa amepokea kiasi fulani.

Condoms zipo na zimeingia leo kulikuwa na ukosefu kwa kiasi fulani kwa maana shule ikifungwa watu huja huzichukuwa kabisa

 

Maelfu ya wajumbe wanaohudhuria mkutano huu, wametakiwa kuwa Makini katika mienendo yao, katika eneo hili ambalo ni miongini mwa kaunti zenye maambikizi makubwa ya Ukimwi nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.