Pata taarifa kuu

Covid 19 inavyorudisha nyuma jitihada za kupambana na Kifua Kikuu

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu TB  na zikuwa  zimesalia miezi michache kabla makataa ya kumaliza ugonjwa wa kifua kikuu ,kufikia mwaka wa 2022, kama walivyoahidi viongozi wa dunia  janga la Corona hata hivyo linatishia kurudisha nyuma hatua zilizopigwa kuafikia lengo hilo.

Bacteria wa wanaosababisha ugonjwa kifua kikuu TB
Bacteria wa wanaosababisha ugonjwa kifua kikuu TB Domaine public
Matangazo ya kibiashara

Nchini Kenya wagonjwa wengi wa TB wamekuwa wanasita kupata matibabu  kutokana na unyanyapaa  na kwamba dalili za Covid 19 zinakaribiana na zile za TB.

Jeniffer Mwandawiro mkazi wa Voi kaunti ya Taita Taveta ,ambaye ni mhudumu wa afya aliyenusurika kujitoa uhai kutokana na  kunyanyapaliwa alipogundulika ana TB.

Wakanipigia simu ,wewe  ndio Jennifer ,nkasema ndio ,sisi ni watu kutoka Lab ,hebu rudi,haya majibu si yako.Kurudi nikapata kila mtu anachokora kutafuta barakoa,nikashindwa kwani nina nini? Wakaniambia nina TB sugu na ni tishio kwa jamii.”

Nilimpigia mamangu simu ,nikamwambia ,ninvyoona nitajitupa  Nyali bridge, ,wananiambia siwezi kaa karibu na mtoto  ,nisikae karibu na watu .

Unyanyapaa unaohusishwa na Corona ugonjwa wenye dalili kama za kifua kikuu ,linazidi kutishia mapambano dhidi ya  TB.

 

Gregory   Mutwiwa baba wa watoto wawili  wanaoendelea na kutibiwa kifua kikuu ,alilazimika kutibu Malaria ,Pheumonia , na magonjwa mengine, isitoshe ,kupata vipimo vya Covid 19  kabla mwanae wa miaka sita kubainika ana kifua kikuu.

 Malaria imeisha lakini bado joto halishuki. Kulikuwa pia na Pneumonia  ,Amoeba na Typhoid,hivyo akaanza tena matibabu  ya siku tatu , baada ya siku tatu ,alipopimwa ,hayo yakuwa yamedidimia lakini bado mtoto alikuwa anatokwa jasho. Akapigwa scan ,wakaona kitu kama wingu jeupe ,tukapewa chaguo la kupima Covid na TB . Covid ilisoma negative.

Daktari kusoma ,na nilipokuwa namwelezea dalili ,mtoto anatokwa jasho,hali, akathibitishwa ni wa kuwekwa kwenye matibabu ya TB.

Ndani ya  juma  moja  mwanae  wa pili mwenye umri wa miaka minne sasa ,naye kathibitishwa ana TB kwa hiyo ikabidi familia nzima ipimwe TB.

Daktari  Philip Owiti  kutoka kituo cha kitaifa cha  kupambana na TB ,anaafiki kuwa hili limekuwa changamoto kubwa.

 Kuna jumbe ambazo zinasema ukiwa unakohoa ,usiende hospital ,piga hii nambari.Jamii ikachukulia ukiwa unakohoa,kuna uwezekano mkubwa una Covid. Sasa watu waliokuwa na TB wakaanza kujificha,hutaki kukohoa mbele ya watu kwa kuwa itasemekana una Covid. Hili limekuwa kikwazo kubwa. Wahudumu wa afya tunawaambia wagonjwa wote wenye dalili za Corona

Mashirika yanaongoza mapambano ya TB pia yanaonya kuwa serikali nyingi zimeelekeza juhudi zote kwenye COVID 19, na kusahau TB ambayo pia  inachangia vifo vya wengi .

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.