Pata taarifa kuu

Covid-19: Kusambaa tena kwa Omicron kunatishia kuanza tena kwa safari za ndege

Aina mpya ya kirusi cha Omicron inatishia kuanza tena hatua kwa hatua safari za ndege, sekta iliyoathiriwa sana na janga hili, ikiwa ni pamoja na ndege zilizopigwa marufuku kuruka mnamo mwaka 2020.

Kwa jumla, abiria milioni 514 walisafiri kwa ndege huko Ulaya mwaka wa 2021, sawa na chini ya robo ya safari za ndege duniani.
Kwa jumla, abiria milioni 514 walisafiri kwa ndege huko Ulaya mwaka wa 2021, sawa na chini ya robo ya safari za ndege duniani. REUTERS - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Tangu mwanzoni mwa mwezi wa Januari, Shirika la Usalama wa Anga la Umoja wa Ulaya, EASAl, limebaini kupungua kwa idadi ya safari za ndege , na kuongeza ni vivyo hivyo huko Marekani.

Nchini Marekani, Shirika la Ndege la Delta limelazimika kusitisha safari zaidi ya 30,000 za ndege tangu Krismasi kutokana na kuenea kwa virusi vya Omicron. Kampuni hiyo ya Marekani imerekodi hasara ya jumla ya dola milioni 408 katika kipindi ncha mwaka mmoja, katika muktadha wa kupanda kwa bei ya mafuta. shirika la ndege la Delta Airlines, hata hivyo, limesema Omicron ilisababisha kufutwa tu kwa 1% ya safari zake za ndege wiki iliyopita na ina matumaini kuwa hali huenda ikawa hivyo mwaka huu wa 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.