Pata taarifa kuu

Mahakama ya Juu yazuia wajibu wa kutoa chanjo katika makampuni, kikwazo kwa Biden

Mahakama ya Juu ya Marekani sikuya Alhamisi ilizuia ombi la hatua ya rais Biden inayotaka wafanyakazi wa kampuni kubwa kupewa chanjo dhidi ya Covid-19 au kufanya vipimo vya mara kwa mara. Majaji waliona hatua hiyo kuwa isiyofaa katika maisha ya Wamarekani wengi.

Rais Joe Biden mbele ya wanahabari baada ya mkutano na maseneta kutoka chama cha Democratic, Alhamisi hii, Januari 13, 2022 huko Washington.
Rais Joe Biden mbele ya wanahabari baada ya mkutano na maseneta kutoka chama cha Democratic, Alhamisi hii, Januari 13, 2022 huko Washington. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Wajibu huu wa chanjo, Ikulu ya White House ilitaka kulazimisha wafanyakazi milioni 84 wanaofanya kazi katika kampuni zenye wafanyikazi zaidi ya 100. Vinginevyo, haiwezekani kufanya kazi isipokuwa ufanye vipimo vywa Covid kila wiki kwa gharama ya mganyakazi mwenyewe.

Hatua hii iliyotangazwa mwezi Septemba na Joe Biden ilishutumiwa mara moja na wabunge na maseneta wa chama cha Republican na kuichukulia kama ya kibabe na kupiganwa mahakamani.

Mahakama ya Juu ilishughulikia suala hilo kwa dharura na kati ya wajumbe wake tisa ni mahakimu watatu tu waliopiga kura ya kuunga mkono, majaji wake sita wa kihafidhina wote walizuia uamuzi huo.

Wajibu huu unaipa motisha mahakama ya juu zaidi ya Marekani katika hukumu yake, "sio matumizi ya kila siku ya mamlaka ya shirikisho, lakini kuingilia maisha na afya ya idadi kubwa ya wafanyakazi".

Majaji wawili wa Kihafidhina waliungana na wenzao kwa kupiga kura ya kuidhinisha wajibu wa chanjo kwa wafanyakazi katika sekta ya afya wanaonufaika na fedha za shirikisho.

Kipingamizi kingine cha kisiasa ambacho kilimuangusha Joe Biden ambaye mara moja alisema "amesikitishwa" kwamba mahakama ilizuia "uamuzi huu muhimu ambao unaweza kuokoa maisha ya watu wengi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.