Pata taarifa kuu

Kristalina Georgieva ashikilia wadhifa wake kama mkuu wa Shirika la Fedha Duniani

Kristalina Georgieva, raia wa Bulgari, bado anaendelea kushikiliwa wadhifa wake kama mkuu wa wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, baada ya kupata uungwaji mkono wa bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Fedha Duniani, Jumatatu wiki hii.

Kristalina Georgieva, Mkuu wa shirika la Fedha Duniani, IMF.
Kristalina Georgieva, Mkuu wa shirika la Fedha Duniani, IMF. AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Kristalina Georgieva alikuwa anashumiwa kupotosha ripoti ya kuipendelea China wakati alikuwa katika Benki ya Dunia. Madai ambayo amekuwa akikanusha kila wakati.

Uongozi wa Bi Georgieva, 68, katika shirika la Fedha Duniani, ulikumbwa na sintofahamu katikati ya mwezi Septemba, baada ya kuchapishwa kwa uchunguzi wa ofisi ya wanasheria kutoka Marekani, WilmerHale, uliofanywa kwa ombi la kamati ya maadili ya Benki ya Dunia. Mkurugenzi Mkuu wa IMF alishtakiwa kwa kudanganya ripoti ya kuipendelea China. Kulingana na watu waliowasilisha mashtaka hayo, alifanya ushawishi, wakati alikuwa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia, ili China isiwekwi kwenye sehemu kadhaa katika ripoti ya Doing Business ya mwaka 2018. Ripoti hii inaweza kuwa na athari kwa mvuto, kwa sababu inaweka kiwango cha nchi katika mazingira mazuri ya biashara.

Jumatatu jioni, "Bodi ya Utendaji (IMF) iligundua kuwa habari iliyowasilishwa wakati wa ukaguzi haikuonyesha kabisa kwamba Mkurugenzi Mkuu alichukua jukumu lisilofaa kuhusu ripoti ya + Doing Business 2018+ wakati alikuwa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia, kulingana na taarifa ya IMF.

Bi.Georgieva, Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Benki ya Dunia, alichukua nafasi ya mkuu wa IMF mnamo Oktoba 1, 2019, akichukua nafasi ya Mfaransa Christine Lagarde aliyeteuliwa katika Benki Kuu ya Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.