Pata taarifa kuu

Nchi za Kusini zatia wasiwasi juu ya kushiriki mkutano wa COP26 Glasgow

Ikiwa zimesalia siku zisizozidi 60 kabla ya mkutano wa 26 wa kimataifa wa mbadiliko ya tabianchi (COP26) kufanyika huko Glasgow, nchini Scottland, nchi masikini zaidi zinajiuliza ikiwa uwepo wao katika mkutano huu ni muhimu kwa dunia, na kwanza kabisa kwa nchi hizi zinazokabiliwa na joto kali, itawezekana, kutokana itifaki za kiafya na kidiplomasia zinazoombwa

Wanaharakati wakiandamana huko London, Julai 23, 2021, siku 100 kabla ya kuanza kwa COP26 huko Glasgow.
Wanaharakati wakiandamana huko London, Julai 23, 2021, siku 100 kabla ya kuanza kwa COP26 huko Glasgow. REUTERS - PETER NICHOLLS
Matangazo ya kibiashara

Sababu ya wasiwasi huu: ugumu wa kufika huko Glasgow, mahali kutakofanyika mkutano huo, kwa sababu ya ukosefu wa chanjo na karantini yenye gharama kubwa iliyowekwa na Uingereza.

Mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali yamekosoa kutofaulu kwa nchi tajiri kusaidia upatikanaji wa chanjo katika nchi masikini na yana hofu kuwa mkutano huo hautakuwa "wa haki na wazi". "Ikiwa imesalia miezi miwili tu, ni dhahiri kwamba mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa salama, unaojumuisha na wa haki hauwezekani, kutokana na kushindwa kusaidia upatikanaji wa chanjo kwa maelfu ya watu katika nchi masikini, kupanda kwa gharama za kusafiri na malazi na kutokuwa na uhakika juu ya kuibuka kwa janga la Covid-19, ” umesema muungano unaojumuisha mashirika 1,500, yakiwemo Greenpeace, WWF, Action Aid, Oxfam au Amnesty International.

Nchi saba tajiri duniani za G7 zinaunga mkono hatua za pamoja za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaojadili swala la mabadiliko ya tabia nchi COP26 utakaofanyika nchini Scottland mnamo mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.