Pata taarifa kuu

Covid-19: Mashirika 1,500 yataka kuahirishwa kwa mkutano wa COP26

Kiwango cha chini cha chanjo kwa nchi nyingi kitasababisha, kutokuepo na usawa katika kusiriki mkutano wa 26 wa kimataifa wa mbadiliko ya tabianchi (COP26), utakaofanyika mwezi Novemba mjini Glasgow, Scottland.

Nchi saba tajiri duniani za G7 zinaunga mkono hatua za pamoja za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaojadili swala la mabadiliko ya tabia nchi COP26 utakaofanyika nchini Scottland mnamo mwezi Novemba.
Nchi saba tajiri duniani za G7 zinaunga mkono hatua za pamoja za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaojadili swala la mabadiliko ya tabia nchi COP26 utakaofanyika nchini Scottland mnamo mwezi Novemba. Jonathan Nackstrand AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na chanjo dhaifu kwa nchi masikini dhidi ya Covid-19, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotetea mazingira yanataka kuahirishwa kwa mkutano huo, yakibaini kwamba "haiwezekani" kufanya mkutano "wa haki na unaojumuisha" watu wote huko Glasgow mwezi Novemba.

"Ikiwa imesalia miezi miwili tu, ni dhahiri kwamba mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi  hauwezekani, kutokana na kushindwa kusaidia upatikanaji wa chanjo kwa maelfu ya watu dunianii. Nchi masikini, kupanda kwa gharama za kusafiri na malazi, na kutokuwa na uhakika kuhusu mabadiliko ya janga la Covid-19, ” limeandika kundi la Climate Action Network, linalojumuisha mashirika 1,500, ikiwa ni pamoja na Greenpeace, WWF, Action Aid, Oxfam na Amnesty International.

Nchi saba tajiri duniani za G7 zinaunga mkono hatua za pamoja za kukabili athari za mabadiliko ya tabia nchi kabla ya mkutano wa Umoja wa Mataifa utakaojadili swala la mabadiliko ya tabia nchi COP26 utakaofanyika nchini Scottland mnamo mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.