Pata taarifa kuu
UNHCR-WAKIMBIZI

Watu Milioni 55 wayatoroka makazi yao kufuatia matatizo mbalimali duniani

Machafuko na majanga ya asili yalisababisha watu Milioni 55 kuyakimbia makwao na kuwa wakimbizi wa ndani katika nchi zao mwaka uliopita, kote duniani.

Wafanyakazi wa shirika la MSF wanaelekeza wakimbizi kutoka Somalia kwenda kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab mashariki mwa Kenya Agosti 1, 2011.
Wafanyakazi wa shirika la MSF wanaelekeza wakimbizi kutoka Somalia kwenda kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab mashariki mwa Kenya Agosti 1, 2011. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya pamoja iliyotolewa na shirika la  Kimataifa linaloshughulikia wakimbizi wa ndani duniani na lile la wakimbizi kutoka nchini Norway, imeeleza kuwa, watu hao walikuwa wakimbizi wa ndani katika nchi zao, licha ya kuwepo kwa masharti ya kupambana na janga la Corona katika mataifa mbalimbali.

Mwaka 2020, ulishuhudia watu wengine wapya Milioni 40.5 wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi zao kufuatia machafuko, mashambulizi na majanga ya asili kama vimbunga na mafuriko.

Hii ndio idadi kubwa ya watu kuwahi kuripotiwa kuwa wakimbizi katika nchi zao ndani ya miaka 10 iliyopita.

Mkurugenzi wa Shirika linaloshughulika na wakimbizi nchini Norway Jan Egeland amesema hii ni ishara kuwa dunia imeendelea kushindwa kuwalinda watu wanaokumbwa na machafuko na majanga ya kiasili.

Vimbunga vilivyotokea hasa katika nchi za bara Asia, vimeelezwa na watalaam kuwa ni kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi, huku mataifa kadhaa ya Afrika, Syria na Afganistan, yakishuhudia raia wake wakikimbia makwao kwa sababu ya utovu wa usalama na mashambulizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.