Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINA-Usalama

Israeli: serikali imeagiza mpango wa ujenzi wa nyumba 1000 Jerusalem

Serikali ya Israeli imesema inaendelea na ujenzi wa makaazi elfu moja Mashariki mwa Mji wa Jerusalem eneo ambalo Palestina inataka kuwa sehemu yake.

Moja ya nyumba ziliyojengwa katika eneo la walowezi la Har Homa karibu na mji wa Jerusalem, Oktoba 27 mwaka 2014.
Moja ya nyumba ziliyojengwa katika eneo la walowezi la Har Homa karibu na mji wa Jerusalem, Oktoba 27 mwaka 2014. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huo wa Israeli ni kinyume na sheria za kimataifa, na unakuja wakati ambapo mji huo wa jerusalem unaendelea kushuhudia hali ya machafuko.

Israeli imeongeza pia kuwa, makaazi mengine yatajengwa katika ukingo wa Magharibi kutumiwa na Waisraeli na Wapelestina.

Jibril Rajoub, Mshirika wa karibu wa rais wa Palestina t Mahmud Abbas amesema ujenzi huo mpya huenda ukasababisha vita.

Israeli imekuwa ikisisitiza kuwa haiwezi kuiachia mji wa Jerusalem kutokana na sababu za kihistoria, dini na usalama, lakini Palestina inasema Mashariki mwa mji huo ni sehemu yake.

Wakaazi wa mji wa beit Hanina wameelezea kukerwa na uchokozi wa Israeli wa kuanzisha ujenzi katika maeneo ambayo si milki yake.

Serikali ya Palestina imelani uamzi huo wa Israeli na kusema kwamba ni uhalifu wakati ambapo Umoja wa Ulaya umeomba rasmi israeli kurejelea hatua yake. Katika hotuba yake mbele ya Bunge la Ulaya Jumatatu Oktoba 27, waziri mkuu wa Israel aliahidi kwamba serikali yake itaendelea na ujenzi katika mji huo mtakatifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.