Pata taarifa kuu
UINGEREZA-PALESTINA-ISRAEL-Siasa

Uingereza: wabunge wapiga kura kama ishara ya kulitambua taifa la Palestina

Wabunge wa Uingereza wamepiga kura kutambua taifa la Palestina, linalopakana na Israel. Kura hizo ziliyopigwa ni ishara kwamba kuna baadhi ya raia nchini Uingereza, wanaoitambua Palestina kama taifa huru.

Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron akikumbusha kwamba kura ziliyopigwa na wabunge kwa kulitambua taiafa la Palestina hazina nguvu yoyote kwa serikali yake.
Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron akikumbusha kwamba kura ziliyopigwa na wabunge kwa kulitambua taiafa la Palestina hazina nguvu yoyote kwa serikali yake. REUTERS/UK Parliament via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Lakini hali hio haitozuia chochote katika siasa za nje za David Cameron, na vilevile haitoishinikiza serikali yake kuitambua Palestina kama taifa huru.

Hata hivyo, nusu ya wabunge hasa wa chama cha Labour ndio walioshiriki katika uupigaji kura huo ambao unasema utasaidia upatikanaji wa suluhu kati ya Palestina na Israel.

Wabunge 274 walipiga kura ya kuunga mkono huku 12 wakipiga kura ya kutoitambua Palestina kama taifa huru.

Bunge la Uingereza linaundwa na wawakilishi wa raia 650, ikimaanisha kwamba idadi ya wabunge waliopiga kura ya kuitambua Palestina kama taifa huru, ni ndogo ikilinganishwa na idadi hiyo ya wabunge wa Bunge la Uingereza.

Mawaziri pia walisusia upigaji kura huo.

Kwa upande wake Waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, amekumbusha kwamba kura hiyo hizo hazina uzito wowote kwa serikali yake aidha kubadili siasa yake ya nje kuhusu suala hilo. Kwa mujibu wa serikali ya Uingereza, Palestina itatambuliwa kufuatia matokeo ya mazungumzo kati ya Israel na Palestina.

Mwaka 2012, Umoja wa Mataifa ulipiga kura na kuitambua Palestina kuwa mwanachama wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.