Pata taarifa kuu
MAREKANI-SYRIA-UTURUKI-IS-KOBANE-Ushirikiano-Mapigano-Usalama

Marekani yapongeza uamzi wa Uturuki

Serikali ya Ankara, imewapa njia wapiganaji wa Kikurdi wa Iraq. Uamzi huo umepongezwa na Marekani, ambayo imeendelea na zoezi lake la kuwashushua silaha kwa njia ya anga wapiganaji wa Kikurdi usiku wa Jumapili kamkia Jumatatu wiki hii.

Wanajeshi wa Uingereza wakitoa mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa Kikurdi (Pershmegas) katika mji wa Arbil nchini Iraq, Oktoba16 mwaka 2014.
Wanajeshi wa Uingereza wakitoa mafunzo ya kijeshi kwa wapiganaji wa Kikurdi (Pershmegas) katika mji wa Arbil nchini Iraq, Oktoba16 mwaka 2014. REUTERS/Azad Lashkari
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo Marekani imeendelea na mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Wiki iliyopita mji wa Kobane ulikua hatarini kudhibitiwa na kundi la wapiganji wa Dola la Kiislam.

Serikali ya Uturuki imesema itawaruhusu wapiganji wa Kikurdi wa Iraq kutumia aridhi yake kwa kuingia katika mji wa Kobane nchini Syria ili waweze kuwasaidi Wakurdi wa Syria wa kundi la PYD, ambalo linaendesha vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Marekani imepongeza pia uamzi huo wa Uturuki, baada ya nchi hiyo kukataa mara kadhaa kusaidia kijeshi mji wa Kobane usidhibitiwe na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Kulingana na taarifa ya mwandishi wa Idhaa ya Kifaransa ya RFI mjini Istanbul, Jérôme Bastion, na wanahabari wengine walioko katika mji huo, hakuna mpiganaji hata mmoja wa Kikurdi ambaye amevuka mpaka wa Uturuki na Syria. Kwa upande wao viongozi tawala katika mji wa Kobane hawajafamisha kuwasili kwa wapiganaji hao. Haijafahamika iwapo ni propaganda wanayo fanyiwa wapiganaji hao wa Kikurdi

Katika uwanja wa mapigano, hali ya utulivu iliripotiwa siku ya Jumapili Oktoba 19 katika mji wa Kobane, lakini mashariki mwa jimbo la Kobane wapiganaji wa Kikurdi wameendelea kudhibiti maeneo yaliyokua yakikaliwa na wapiganaji wa Dola la Kiislam, baada ya kutimka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.