Pata taarifa kuu
MAREKANI-UTURUKI-IS-PKK-KOBANE-Ushirikiano-Mapigano-

Syria: Marekani yawapa silaha wapiganaji wa Kikurdi

Jeshi la Marekani limewapatishia silaha na dawa kwa njia ya anga waasi wa kikurdi wanaopambana na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam katika mji wa kobane uliozingirwa na wapiganaji wa kundi hilo tangu kwa majuma kadhaa sasa.

Mkaazi wa mji wa Kobane kutoka jamii ya Wakurdi akiangalia ndege za kivita katika anga ya mji wa Kobane zikitokea kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.
Mkaazi wa mji wa Kobane kutoka jamii ya Wakurdi akiangalia ndege za kivita katika anga ya mji wa Kobane zikitokea kwenye mpaka wa Uturuki na Syria. AFP PHOTO/BULENT KILIC
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya kijeshi ya mizogo C130 imewashushia silaha kwa njia ya anga wapiganaji wa Kikurdi wanaoendelea kumudu mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam waliouzungira mji wa Kobane.

Hatuwa hii huenda ikapokelwa vibaya na Uturuki, wakati huu Marekani na washirika wake katika muungano dhidi ya Kundi la hilo wakiendelea kuishinikiza Uturuki kushiriki kikamilifu katika operesheni za muungano.

Hata hivyo serikali ya Ankara imekuwa ikisita kuhusu swala la kuwapa silaha waasi wa Kikurdi katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, kutokana na kuwatuhumu waasi hao kuwa miongoni mwa makundi ya kigaidi ya PKK yanayo pambana na serikali tangu zaidi ya miaka 30 wakidai mjitengo wa eneo la kusini mashariki kujitenga na Uturuki.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imefahmisha kwamba viongozi wa Marekani walikutana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa Juma na viongozi wa wa Kikurdi wa Syria wa Chama cha PYD kinacho miliki wapiganaji wa PKK ambao serikali ya Ankara imewarodhesha katika makundi ya Kigaidi.

Kulingana na taarifa kutoka jeshi la Marekani, mashambulizi ya anga ya vikosi vya muungano yamewasaidia wapiganaji wa Kikurdi kuwarejesha nyuma wapiganaji wa Dola la Kiislam Jumamosi na jumapili mwishoni mwa juma liliyopita katika jaribio la kutaka kusonga mbele kwenye uwanja wa mapambano.

Haijafahamika iwapo silaha hizo na dawa vimewafikia wapiganaji wa Kikurdi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.